Mfumo wa 1,000 wa kuendesha gari lenye uwezo wa kuruka angani la ARIDGE watoka kwenye mstari wa uzalishaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 12, 2026
Mfumo wa 1,000 wa kuendesha gari lenye uwezo wa kuruka angani la ARIDGE watoka kwenye mstari wa uzalishaji
Wafanyakazi wakikagua hali ya uendeshaji wa mkono wa roboti ndani ya karakana ya uundaji wa jumla ya kiwanda cha ARIDGE cha uundaji wa wingi wa magari yenye uwezo wa kuruka angani, huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Agosti 10, 2026. (Xinhua/Deng Hua)

Hafla ya kukamilika na kutoka kwenye mstari wa uundaji wa seti ya 1,000 ya mfumo wa umeme wa kuendesha gari lenye uwezo wa kuruka angani la ARIDGE, ambalo pia linajulikana kwa jina la " Manowari ya Ardhini," ilifanyika kwenye kiwanda cha kampuni hiyo cha uundaji wingi wa magari yenye uwezo wa kuruka angani katika Mji wa Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China Jumatatu wiki hii.

Kampuni ya ARIDGE ni muundaji mwanzilishi wa mpango wa usafiri wa anga ya chini yenye makao yake makuu mkoani Guangdong. Kiwanda cha uundaji wingi wa magari yenye uwezo wa kuruka angani katika mji wa Guangzhou, eneo lake linafikia mita za mraba takriban 120,000, hasa kinaunda sehemu yenye uwezo wa kurukia angani ya gari hiyo inayosifiwa kuwa ya "Manowari ya Ardhini."

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha