Lugha Nyingine
Idadi ya vifo katika tetemeko la ardhi nchini Colombia yaongezeka hadi 132, zaidi ya 570 wajeruhiwa (2)
![]() |
| Rais wa Colombia Abelardo de la Espriella akihudhuria mkutano wa kukabiliana na tetemeko la ardhi mjini Bogota, mji mkuu wa Colombia, Agosti 10, 2026. (COLPRENSA/kupitia Xinhua) |
BOGOTA - Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 lililotokea magharibi mwa Colombia jana Jumatatu imeongezeka hadi kufikia 132, huku wengine zaidi ya 570 wakijeruhiwa, serikali ya Colombia imesema katika taarifa yake ya hivi punde zaidi mapema leo Jumanne.
Kwa mujibu wa ripoti ya awali, miji 32 kote nchini humo imeathiriwa vibaya, wakati miji mikuu mitano ya kiidara -- Pereira, Cali, Quibdo, Manizales na Armenia -- ikiendelea kuwa chini ya tahadhari kali. Ripoti hiyo imesema Mji wa Pereira umeripoti vifo 60, ukifuatiwa na Cali wenye vifo 15, Quibdo wenye vifo 8 na Manizales wenye vifo vinne.
Taarifa imesema kwa jumla majengo 86 yameporomoka, huku huduma zikisimamishwa katika viwanja 7 vya ndege kwa sababu ya hasara iliyosababishwa na tetemeko hilo la ardhi.
Serikali ya Colombia mapema jana Jumatatu ilitangaza hali ya janga la kitaifa ili kukabiliana na athari za tetemeko hilo la ardhi.
Kwa mujibu wa Huduma ya Jiolojia ya Colombia, tetemeko hilo lilitokea saa 1:34 asubuhi kwa saa za huko magharibi mwa Colombia. Eneo ambako lilianzia na kuleta athari kubwa zaidi ni karibu na San Jose del Palmar, katika idara ya Choco, kwa kina cha kilomita 96.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




