Wakulima wa chai wavuna chai ya Longjing ya Ziwa Xihu ya Hangzhou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2026
Wakulima wa chai wavuna chai ya Longjing ya Ziwa Xihu ya Hangzhou, China
Picha ikionyesha wakulima wa chai wakichuma majani ya chai katika Kijiji cha Meijiawu cha Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Machi 19, 2026. (Xinhua/Xu Yu)

Wakulima wa chai katika maeneo ya Mji wa Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China wameanza kuvuna chai ya Longjing ya Ziwa Xihu, ambayo ni moja ya chai maarufu zaidi nchini China.

Chai ya Longjing ni chai ya kijani. Ikiwa ni moja ya chai 10 maarufu zaidi za China, chai ya Longjing ya Ziwa Xihu inajulikana kwa majani yake ya rangi ya kijani yenye umbo zuri, harufu nzuri ya kipekee, na ladha yake inayojaa harufu za maua na matunda.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha