

Lugha Nyingine
Maonyesho ya Canton yaanza kusini mwa China yakiwa na rekodi ya waonyeshaji na wanunuzi bidhaa
![]() |
Picha hii iliyopigwa Oktoba 15, 2025 ikionyesha Maonyesho ya 138 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. (Xinhua/Deng Hua) |
GUANGZHOU - Maonyesho ya 138 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China, yameanza rasmi jana Jumatano, ambapo idadi ya wafanyabiashara wanaoshiriki kwenye maonesho hayo imezidi 32,000, na kufikia rekodi ya juu, maonesho hayo yamepangwa kufanyika kuanzia Oktoba 15 hadi Novemba 4 katika Mji wa Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, maonyesho hayo ya 138 pia yamevutia idadi kubwa ya wanunuzi.
Waandaaji wa maonesho hayo wamejulisha kuwa, hadi kufikia Jumatatu, wafanyabiashara wa manunuzi wapatao zaidi ya 240,000 kutoka masoko 218 walikuwa wamejiandikisha mapema, ikionesha ongezeko la asilimia 10 ikilinganishwa na maonyesho yaliyopita.
Wamesema, miongoni mwao -- idadi ya wanunuzi kutoka Umoja wa Ulaya, Marekani na nchi zinazoshiriki katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja imeongezeka kwa kiasi kikubwa, huku kampuni zaidi ya 400 za ununuzi zikishiriki kwenye maonyesho hayo.
Utafiti uliofanywa kabla ya maonyesho hayo unaonesha kuwa, bidhaa za aina mpya zaidi ya milioni 1 zilizozalishwa katika mwaka uliopita zitaonyeshwa kwenye maonyesho hayo ya 138, wakati bidhaa karibu 800,000 zitaonyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye maonyesho hayo.
Waandaaji wamesema kwamba, Maonesho hayo ya 138, kwa mara ya kwanza, yameweka eneo la kuonyesha bidhaa za teknolojia za kisasa za matibabu -- ambalo limevutia kampuni 47 zinazoonyesha bidhaa kama vile roboti za upasuaji, mifumo ya ufuatiliaji na udhibiti ya AI na vifaa vya kuvaliwa. Aidha, maonyesho hayo yataendelea kuweka eneo la roboti za kutoa huduma, ambalo limevutia viwanda 46 vya kuongoza sekta ya roboti kuonyesha roboti zao za miundo ya binadamu, mbwa na bidhaa nyingine zilizobuniwa upya. .
Maonesho ya Biashara ya Guangzhou yalianzishwa rasmi mwaka 1957, yanafanyika mara mbili kwa mwaka, ambayo ni maonyesho yanayofanyika kwa muda mrefu zaidi yakiwa na shughuli nyingi zinazohusisha biashara ya kimataifa nchini China, na yamekuwa yakisifiwa kama kipimo cha biashara ya nje ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma