

Lugha Nyingine
Rais Trump wa Marekani apendekeza kuifukuza Hispania kutoka NATO
WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump kwenye mkutano na Rais wa Finland Alexander Stubb aliye ziarani huko Washington, D.C., Marekani amependekeza kuifukuza Hispania kutoka Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) kwa kuwa imekataa kuongeza matumizi yake ya ulinzi.
"Hawana kisingizio cha kutofanya hivi. Kusema kweli huenda mnapaswa kuwatupa nje ya NATO." Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House jana Alhamisi.
"Nyie watu itabidi muanze kuzungumza na Hispania. Inabidi muwaite na mfahamu kwa nini wako nyuma." Trump amesema.
Kutokana na shinikizo kutoka kwa Rais Trump, nchi wanachama wa NATO mwezi Juni zilikubali kuongeza matumizi yao ya kijeshi hadi asilimia 5 ya pato la taifa ifikapo mwaka 2035.
Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez alikataa lengo hilo, akilielezea "lisilooana na ustawi wa nchi yetu na maono yetu ya dunia."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma