

Lugha Nyingine
Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” 2025 lafanyika Kunming
KUNMING – Jukwaa la Ushirikiano la Vyombo vya Habari la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” 2025 limefanyika mjini Kunming, Mkoa wa Yunnan wa China. Zaidi ya wajumbe 200 kutoka nchi na mashirika ya kimataifa na ya kikanda 87, vyombo vya habari na taasisi 165 walishiriki kwenye jukwaa hilo.
Washiriki wameona kuwa, tangu Rais Xi Jinping alipotoa pendekezo muhimu la kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” mwaka 2013, pendekezo hilo limepata matunda mengi, na kuwa bidhaa ya kimataifa ya umma na jukwaa la ushirikiano wa kimataifa linalopendwa na watu wengi. Hivi karibuni, Rais Xi Jinping katika mkutano wa “Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai + (SCO+)” alitoa Pendekezo la Usimamizi wa Dunia, ambalo limetoa hekima ya China na mpango wa China kwa ajili ya kujenga mfumo wa usimamizi wa dunia ulio wa haki na halali zaidi, na pia kufungua nafasi mpya na kubwa zaidi kwa ajili ya ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja.”
Washiriki walisema kuwa, vyombo vya habari vya nchi mbalimbali vinapaswa kuimarisha zaidi ushirikiano, kuwa watendaji na wahamasishaji wa moyo wa Njia ya Hariri, na kufanya juhudi za kueneza mtazamo wa ustaarabu kuhusu usawa, kufundishana, kufanya mazungumzo na ujumuishi; kuwa waandishi na wasimulizi wa mafanikio ya maendeleo, kuendelea kuripoti kwa undani utekelezaji halisi wa ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja," na kukusanya nguvu chanya za ushirikiano wa kunufaishana; na kuwa washiriki na wahimizaji wa kufundishana kwa ustaarabu, kutoa habari na ripoti nzuri kwa kuongeza maelewano, kuvunja hali ya matengano, na kuunganisha nguvu, ili kuimarisha msingi wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Jukwaa hilo limeandaliwa kwa pamoja na Shirika la gazeti la People's Daily, Kamati ya Chama ya Mkoa wa Yunnan, na Serikali ya Mkoa wa Yunnan, ukiwa na kauli mbiu ya "Kubeba kwa pamoja wajibu wa Vyombo vya Habari, Kuhimiza Kufundishana kwa Ustaarabu." Ratiba ilihusisha hafla ya ufunguzi, jukwaa kuu, majukwaa matawi mengi kikiwemo mazungumzo ya ushirikiano wa vyombo vya habari vya "Ukanda Mmoja, Njia Moja," hafla ya kutoa Tuzo ya Pili ya Mawasiliano ya Kimataifa ya "Njia ya Hariri," na kongamano la ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya ASEAN na China, Japan na Korea Kusini (10+3). Baada ya jukwaa hilo, washiriki kutoka vyombo vya habari vya ndani na nje ya China watashiriki katika shughuli za kukusanya habari kwa pamoja katika mkoa wa Yunnan na mikoa mingine nchini China.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014, Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umefanyika mara 9 kwa mafanikio. Wajumbe zaidi ya 1,000 wa vyombo vya habari na mashirika ya kimataifa na ya kikanda kutoka nchi na maeneo zaidi ya 100 wameshiriki kwenye shughuli hiyo kutokana na mwaliko, wakitoa mchango mkubwa kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo ya kiwango cha juu ya ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma