

Lugha Nyingine
Shughuli yenye maudhui ya Wurigong yafanyika katika kijiji cha Kabila la Wahezhe cha Zhuaji, China
Watu wa Kabila la Wahezhe wamefanya shughuli yenye maudhui ya Wurigong kwenye kijiji chao cha Zhuaji katika Mji Mdogo wa Wusu Mjini Fuyuan, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China. Wahezhe ni moja ya makabila yenye watu wachache zaidi nchini China, wanaoishi kando ya Mito Heilongjiang, Songhuajiang na Wusulisa katika Mkoa huo wa Heilongjian. Kutokana na uwepo wao katika sehemu ya mashariki, wanajulikana kwa jina la "watazama jua."
Neno "Wurigong" linamaanisha furaha na sherehe katika lugha ya kabila la Wahezhe. Shughuli hiyo hutumika kama jukwaa la kuonyesha utamaduni wa Wahezhe, ikichanganya muziki wa kijadi, ngoma, sanaa ya hadithi na michezo.
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma