Msichana wa Russia amwokoa mwanamke aliyekuwa akizama wakati wa safari yake ya mahafali mjini Shaoxing, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 26, 2025
Msichana wa Russia amwokoa mwanamke aliyekuwa akizama wakati wa safari yake ya mahafali mjini Shaoxing, China
Gubaidulina Shakhnaz Evgenevna akijisomea katika Chuo Kikuu cha Huzhou katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, tarehe 24 Juni 2025. (Picha na Yi Fan/Xinhua)

Gubaidullina Shakhnaz Evgenevna, msichana wa Russia anayesoma katika Mji wa Huzhou, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China amefuatiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii ya China hivi karibuni. Amehitimu punde tu kutoka Chuo Kikuu cha Huzhou na shahada ya kwanza.

Juni 23, alishuhudia mwanamke mzee akidumbukia majini, wakati akisafiri kuelekea Mji wa Shaoxing wa Mkoa huo wa Zhejiang katika safari yake ya mahafali. Hakusita kuruka majini na kujaribu kumuokoa mama huyo aliyekuwa akizama.

Shukrani kwa juhudi za pamoja za yeye na wakazi walioko kando ya mto, mwanamke huyo mzee alifanikiwa kuokolewa. Mchakato mzima wa Shakhnaz kuokoa maisha ya mwanamke huyo ulinaswa na kamera ya uangalizi na kusambaa kwenye intaneti, na amesifiwa sana na watumiaji wa mtandao.

Shakhnaz alikuja China mwaka 2016. Akiwa amesoma na kuishi nchini China kwa miaka mingi, anapenda sana utamaduni wa China. Shakhnaz ni mshiriki pekee wa kike wa kigeni wa kundi la ngoma ya kijadi ya simba katika chuo kikuu hicho. Ingawa amehitimu kutoka chuo kikuu hicho, Shakhnaz hataki kuondoka Huzhou. Ametuma maombi kwenye Chuo cha shahada ya uzamili cha Chuo Kikuu cha Huzhou na amemaliza usaili wa udahili.

"Ninapapenda hapa sana. Nataka kuendelea kusoma hapa labda kubaki na kuishi hapa," amesema Shakhnaz. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha