Shirika la ndege la China Eastern lazindua njia ya safari ya moja kwa moja kati ya Xi'an na Istanbul (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 25, 2025
Shirika la ndege la China Eastern lazindua njia ya safari ya moja kwa moja kati ya Xi'an na Istanbul
Abiria wakiwa wamepanga foleni kwenye kaunta za Shirika la Ndege la China Eastern ili kupanda ndege ya kwanza ya moja kwa moja kutoka Istanbul hadi Xi'an kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul nchini Uturuki, tarehe 24 Juni 2025. (Xinhua/Liu Lei)

ISTANBUL - Ndege ya Shirika la Ndege la China Eastern iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 200 imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul majira ya saa 1 asubuhi kwa saa za huko (0400 GMT) jana Jumanne, ikimaanisha kuzinduliwa kwa njia mpya ya safari ya moja kwa moja ya shirika hilo kati ya mji wa Xi'an, kusini magharibi mwa China na Mji wa Istanbul wa Uturuki.

Hiyo ni njia ya pili ya moja kwa moja ya shirika hilo la ndege inayounganisha China na Uturuki, kufuatia huduma yake ya Shanghai-Istanbul.

Ikiwa inaendeshwa na ndege ya Airbus A330, njia hiyo mpya inatoa safari tatu za kwenda na kurudi kwa wiki siku za Jumanne, Ijumaa, na Jumapili, kwa mujibu wa shirika hilo la ndege lenye makao makuu mjini Shanghai.

Katika hafla ya uzinduzi wa safari ya kwanza ya kurudi kwenye uwanja wa ndege wa Istanbul jana Jumanne asubuhi, naibu konsuli mkuu wa ubalozi wa China mjini Istanbul Wu Jian, amepongeza kuanzishwa kwa njia hiyo mpya kama hatua muhimu katika kujenga "Njia ya Hariri ya Angani" iliyo rahisi kati ya miji hiyo miwili ya kihistoria.

Wu amesema kuwa njia hiyo mpya itaongeza msukumo mpya katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi, mawasiliano ya kitamaduni, na kujenga kwa pamoja Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kati ya China na Uturuki.

Firat Ocak, mkurugenzi wa maendeleo ya usafiri wa anga katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul, amesisitiza dhamira ya uwanja huo kwa soko la China na kueleza imani yake kuwa njia hiyo mpya itawapa wasafiri wa China njia bora zaidi za usafiri wa kwenda Ulaya na kwingineko kupitia Istanbul.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha