

Lugha Nyingine
Mdundo wa Pamoja na ndoto za Pamoja – mradi wa mawasiliano ya kiutamaduni wazidisha uhusiano kati ya China na Kenya (6)
NAIROBI – Asubuhi ya Jumatano, hali karibu na Chuo Kikuu cha Kenyatta jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ilikuwa ikivuma kwa mdundo na nguvu. Mchanganyiko mzuri wa mila za kale na usanii wa kisasa ulikuwa ukijionyesha wakati wasanii kutoka China na Kenya walipopanda jukwaani, wakitoa onyesho la kiutamaduni la kuvuka mabara.
Shughuli hiyo itafanyika maonyesho zaidi ya 10, ikiwemo maonyesho ya sanaa ya kupigana, muziki wa ala za jadi za China, na kazi bora za kiutamaduni zinazoonyesha ushujaa, umoja na uzuri wa mazingira ya asili.
Wakiwa wamevalia mavazi ya kijadi yenye kupendeza, kikundi cha wasanii wageni 14 kutoka Chuo Kikuu cha Ualimu cha Shandong mashariki mwa China kilionyesha umahiri wao wa ala kama vile gitaa, filimbi na saksafoni, wakisuka sauti za kuvutia ambazo zilitoa mvumo wenye kugusa sana watazamaji.
Watumbuizaji wa Kenya pia waliangaziwa kwenye shughuli hiyo ya nusu siku, wakifanya maonyesho kwa ala za kijadi zinazowakilisha urithi tajiri na anuwai wa makabila nchini humo.
Feng Jikang, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Shandong, amesema kuwa tangu kuzindua mradi wa mawasiliao ya wanafunzi na kukuza vipaji kati yake na Chuo Kikuu cha Kenyatta mwaka 2008, vyuo vikuu hivyo viwili vimekuwa vikitumia nguvu zao bora za kiutamaduni ili kupata mafanikio katika ushirikiano wa kisanii na kitamaduni.
Feng amesema, Maonyesho hayo, yamepokea mwitikio wa shauku kutoka kwa watazamaji wa wenyeji, akisisitiza kwamba shughuli ya mawasiliano kama hiyo huwapa washiriki wa Kenya hisia dhahiri na uzoefu wa moja kwa moja wa utamaduni tajiri wa jadi wa China.
Kufuatia tukio hilo, wanafunzi na walimu wengi wenyeji wameonyesha nia ya kutafuta masomo zaidi nchini China. Feng ameeleza matumaini ya kuwepo mawasiliano zaidi ya kitamaduni na kitaaluma kati ya China na Afrika ili kuzidisha urafiki, kuhimiza mapatano, na kuimarisha uhusiano kati ya watu na watu.
Kwa upande wake, Waceke Wanjohi, naibu mkuu wa chuo anayeshughulikia masuala ya kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, amesema maonyesho hayo yameonyesha uhusiano wa kitamaduni uliodumu kati ya Kenya na China.
"Dunia ni kijiji cha kimataifa. Shughuli kama hiyo zinatusaidia kufungamanisha tamaduni kutoka sehemu mbalimbali za dunia na utamaduni wa Kenya," Wanjohi amesema.
Kikundi hicho cha wasanii wageni kutoka chuo kikuu hicho cha China hadi sasa kimefanya maonyesho sita sehemu mbalimbali nchini Kenya, kikionyesha uzuri wa utamaduni wa China katika vyuo vikuu na kumbi za kitamaduni, kama vile Maktaba ya Taifa ya Kenya. Kuanzia sanaa ya kupigana hadi sauti za kuvutia safari yao imekuwa moja ya midundo ya pamoja na ndoto za pamoja.
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma