Xiaomi yawezesha ukuaji wa magari ya umeme kupitia teknolojia za kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2025
Xiaomi yawezesha ukuaji wa magari ya umeme kupitia teknolojia za kisasa
Lei Jun, mwanzilishi na mwenyekiti wa Xiaomi, akizungumza na wanahabari kwenye kiwanda cha magari cha Xiaomi mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 16, 2025. (Xinhua/Zheng Huansong)

BEIJING - Ndani ya karakana katika kiwanda cha magari yanayotumia nishati ya umeme (EV) cha kampuni kubwa ya kiteknolojia ya China, Xiaomi, hali ni tofauti kabisa na kile ambacho mtu anaweza kutarajia kuona kwenye eneo la kiwanda ambapo wafanyakazi wachache huonekana, mikono ya roboti husogea kwa usahihi na kasi, ikiunganisha bila kukoma sehemu za magari.

Roboti zinazohama Kiotomatiki (AMRs) zinateleza kwenye sakafu, na kusafirisha nyenzo kwa ufanisi hadi kwenye vituo vilivyoteuliwa.

Kampuni hiyo ya Xiaomi iliingia katika soko la EV mwaka 2021, na kuanzisha kiwanda cha kisasa zaidi ambacho kilichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 720,000 katika Eneo la Maendeleo ya Kiuchumi na Teknolojia la Beijing, pia likijulikana kwa jina la Beijing E-Town - kituo muhimu cha uvumbuzi kwa sekta ya magari ya kujiendesha kiotomatiki ya China. Kampuni hiyo mpya katika soko, ilizindua modeli yake ya SU7 mwezi Machi 2024.

Kila baada ya sekunde 76, gari jipya la Xiaomi linatoka kwenye mstari wa uzalishaji kiwandani, huku zaidi ya roboti 700 zikifanya kazi muda wote wa siku ili kuwezesha ufanyaji kiotomatiki kamili wa michakato muhimu kama vile ulainishaji vyumba kwa kiwango kikubwa.

Kiwanda hicho kinabeba maono ya Xiaomi kwa uundaji magari kwa kutumia teknolojia za kisasa, ambapo mashine zenye uwezo wa teknolojia za kisasa zinaongoza na ufanyaji kazi kiotomatiki unaongeza ubora na ufanisi.

Kwa Lei Jun, mwanzilishi na mwenyekiti wa Xiaomi, umuhimu wa uwekezaji endelevu katika uvumbuzi unajidhihirisha.

"Kwa kushikilia kanuni yetu isiyoyumba ya 'kuzingatia teknolojia kama msingi,' Xiaomi imewekeza yuan zaidi ya bilioni 100 (dola za Kimarekani kama bilioni 13.93) kwenye utafiti na maendeleo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na kupiga hatua kubwa katika uwezo wengi wa msingi.

"Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, tumefuata kwa uthabiti mkakati wetu wa hali ya juu," Lei amesema, akiongeza kuwa katikati ya ushindani mkubwa katika soko la magari, Xiaomi inaendelea kudhamiria kwenye kutupia macho siku za usoni - kuimarisha uwezo wake mkuu wa ushindani, kukidhi mahitaji mbalimbali ya watumiaji, na kuendeleza mnyororo wa thamani kwa ushirikiano wa karibu na washirika wa sekta katika soko linalopanuka.

Tangu Machi 2024, Xiaomi imewasilisha kwa wateja magari zaidi ya 250,000, kwa haraka ikiibuka kuwa mdau muhimu katika soko la magari yanayotumia nishati mpya linalokua kwa kasi nchini China kwa kutumia uundaji magari kwa teknolojia ya hali ya juu na mazingira mazuri ya sera ili kuongeza kasi yake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha