

Lugha Nyingine
Watu wawili wanaoshukiwa kuwa magaidi wauawa katika mlipuko wa bomu nchini Uganda
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2025
![]() |
Picha hii iliyopigwa Juni 3, 2025 ikionyesha eneo la mlipuko wa bomu ambao ulitokea mapema karibu na kanisa katika eneo la Munyonyo, kitongoji cha Kampala, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua) |
KAMPALA - Jeshi la Uganda limesema kuwa limeua watu wawili wanaoshukiwa kuwa magaidi waliokuwa wamebeba kilipuzi katika mji mkuu Kampala, ambapo Chris Magezi, msemaji wa jeshi hilo ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwa njia ya simu jana Jumanne kwamba bomu hilo lililipuka katika wakati wa kuwakamata washukiwa hao wawili.
"Mmoja alikuwa mlipuaji wa kujitoa mhanga, binti," Magezi amesema, akiongeza kuwa wawili hao walikuwa wakipanda pikipiki katika eneo la Munyonyo, kitongoji cha Kampala.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma