Mashindano ya umahiri wa lugha ya Kichina yafanyika Malta (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 08, 2025
Mashindano ya umahiri wa lugha ya Kichina yafanyika Malta
Mwanafunzi akifanya onyesho la mavazi ya Kichina kwenye raundi ya nchi ya Malta ya Mashindano ya 24 la umahiri wa Lugha Kichina ya "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya kigeni katika Chuo Kikuu cha Malta mjini Msida, Malta, Mei 7, 2025. (Xinhua/Chen Wenxian)

VALLETTA - Wanafunzi sita kutoka Chuo Kikuu cha Malta wameonyesha ujuzi na vipaji vyao vya lugha ya Kichina jana Jumatano kwenye raundi ya nchi ya Malta ya Mashindano ya 24 ya umahiri wa Lugha ya Kichina ya "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya kigeni.

Mashindano hayo yaliyofanyika katika chuo kikuu hicho na kuandaliwa na Taasisi ya Confucius, yametoa jukwaa kwa wanafunzi kueleza mapenzi yao kwa lugha ya Kichina na kueleza ndoto zao za kuitembelea China.

Kufuatia hotuba zao zilizotolewa kwa lugha ya Kichina, washiriki waliimba nyimbo za Kichina, kupiga muziki wa Kichina kwa piano au filimbi, kucheza michezo ya kufumba kivuli au kusoma shairi la Kichina. Maonyesho hayo yalivutia watazamaji, ambao walipiga makofi ya furaha kwa kuwapongeza.

Marie Claire Aquilina ameshinda tuzo ya nafasi ya kwanza katika mashindano hayo na atasafiri nchini China kuwakilisha Chuo Kikuu cha Malta kushiriki katika fainali za kimataifa. Kwa sasa Aquilina anasoma shahada ya uzamili katika utafsiri na anatumai siku moja kufanya kazi ya kutafsiri kutoka lugha ya Kichina kwenda Lugha ya Kimalta, au kuwa mwalimu wa lugha ya Kichina.

Mshindi wa nafasi ya pili Matilde Ferrario pia ana fursa ya kutembelea China. "Kujua lugha ya Kichina kutanisaidia sana katika kutafuta kazi yangu ya baadaye," amesema Ferrario, ambaye anatarajia kujiingiza katika kazi za utalii.

Dennis Mizzi, mkurugenzi wa kigeni wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Malta, ameelezea matumaini yake kwamba wanafunzi zaidi watachukua masomo ya lugha ya Kichina.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha