Raia 26 wameuawa, 46 kujeruhiwa baada ya makombora ya India kushambulia nchini Pakistan (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2025
Raia 26 wameuawa, 46 kujeruhiwa baada ya makombora ya India kushambulia nchini Pakistan
Picha iliyopigwa kwa simu janja Mei 7, 2025 ikionyesha jengo lililobomolewa katika shambulizi la kombora la India mjini Muzaffarabad, Kashmir inayodhibitiwa na Pakistan. (Str/Xinhua)

ISLAMABAD - Watu zaidi ya 26 waliuawa na wengine 46 walijeruhiwa baada ya India kupiga makombora dhidi ya maeneo sita nchini Pakistan, amethibitisha Ahmed Sharif Chaudhry, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Umma (ISPR) ya Jeshi la Pakistan Luteni Jenerali katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumatano.

Katika taarifa ya video iliyotolewa mapema, Luteni Jenerali Ahmed, mkurugenzi mkuu wa ISPR, ambalo ni tawi la vyombo vya habari la Jeshi la Pakistani, amesema kwamba India imefanya mashambulizi 24 dhidi ya maeneo sita ya kiraia.

Chaudhry amesema kuwa mashambulizi hayo ya India yamebomoa misikiti minne na kuharibu vibaya nyumba kadhaa na hospitali moja.

Mkurugenzi huyo mkuu amesema kuwa makombora hayo yalilenga maeneo ya Bahawalpur, Sialkot, Shakargarh na Sheikhupura katika Jimbo la mashariki la Punjab, vilevile wilaya za Muzaffarabad na Kotli katika Jimbo la Kashmir linalodhibitiwa na Pakistan.

Mkuu huyo wa ISPR amesema kuwa ndege za Jeshi la Anga la Pakistan zilikuwa angani na kuhakikisha kuwa hakuna ndege ya India inayoshambulia anga ya Pakistan, akiongeza kuwa makombora hayo yalirushwa kutoka ndani ya anga ya India.

"Niseme bila shaka: Pakistan itajibu hili (shambulizi) kwa wakati na mahali itakapochagua. Uchokozi huu hautapita bila kujibiwa," amesema.

Hali ya hatari imetangazwa kwenye hospitali katika maeneo yote yaliyoathiriwa, wakati huohuo Pakistan ilikuwa imesimamisha anga yake kwa saa 48 na kufunga taasisi za elimu jimboni Punjab.

Mkurugenzi mkuu huyo amesema kuwa Jeshi la Anga la Pakistan na Jeshi linajibu ipasavyo shambulizi hilo la India.

Waziri wa Ulinzi wa Pakistan Khawaja Asif amedai kuwa Pakistan imetungua ndege tano za kivita za India na droni tatu katika kujilinda kwake kwa mujibu wa sheria za kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa.

Awali, ofisi ya mambo ya nje ya Pakistan ililaani vikali mashambulizi hayo ya makombora yaliyofanywa na India mapema Jumatano katika maeneo ya raia nchini Pakistan, yakiwemo maeneo ya Kashmir inayodhibitiwa na Pakistan, ikiyaita kuwa ni kitendo cha uvamizi wazi bila sababu yoyote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha