

Lugha Nyingine
Uhusiano kati ya China na EU una ushawishi mkubwa zaidi duniani katika dunia yenye misukosuko: Makamu Rais wa China (3)
![]() |
Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na wawakilishi wa balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini China kabla ya kuhudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 6, 2025. (Xinhua/Li Tao) |
BEIJING - Chini ya hali ilivyo sasa ya msukosuko ya kimataifa, uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya (EU) unashikilia umuhimu mkubwa unaozidi kuongezeka wa kimkakati na ushawishi wa kimataifa, Makamu Rais wa China Han Zheng amesema jana Jumanne alipokuwa akihutubia hafla ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Umoja wa Ulaya mjini Beijing.
Han amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya miaka 50 iliyopita, mawasiliano na mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamezidi kuwa karibu, mafungamano ya maslahi yamezidishwa, kiwango cha ushirikiano vimeinuka sana, jambo ambalo limehimiza maendeleo ya pande zote mbili, na kunufaisha dunia.
“Hakuna mgongano wa maslahi ya kimsingi au migogoro ya siasa za kijiografia kati ya China na EU, ikizifanya washirika ambao wanaweza kunufaishana,” Han amesema.
Amesema pande zote mbili zinapaswa kutumia fursa iliyotolewa na maadhimisho hayo ya miaka 50 ya uhusiano wao, kushikilia nia zao za awali katika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia, kufanya kazi kufahamu kwa usahihi mwelekeo wa jumla wa uhusiano wao, kutilia maanani msimamo uliowekwa wa ushirikiano wao, kuhimiza kila mara maendeleo mazuri ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, na kushikilia kanuni za kuheshimiana, kufungua mlango na kushirikiana, na vilevile kunufaishana.
Kabla ya hafla hiyo, Han alikutana na Rais wa zamani wa Baraza la Ulaya Charles Michel na wawakilishi wa balozi za Umoja wa Ulaya nchini China, akisema kuwa China na EU zimerejesha kikamilifu mawasiliano kati ya mabunge yao, ikitoa msukumo mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.
“Zikikabiliana na hali ngumu na tete ya kimataifa, China na Umoja wa Ulaya, zikiwa nguvu kubwa mbili zinazobeba jukumu la kuleta utulivu na la kiujenzi duniani, zinapaswa kubeba wajibu wao, kuimarisha mazungumzo, kuzidisha ushirikiano, kushughulikia tofauti za kiuchumi na kibiashara ipasavyo, na kufanya kazi pamoja kulinda kanuni na utaratibu wa biashara wa pande nyingi,” Han amesema.
Upande wa EU umesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 50 iliyopita, uhusiano wa EU na China umekuwa moja ya uhusiano wa karibu zaidi duniani na kwamba pande zote mbili zinapaswa kupitia na kufanya majumuisho ya uzoefu wao, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, kuweka msingi thabiti kwa maendeleo zaidi ya uhusiano kati ya EU na China katika kipindi cha miaka 50 ijayo, na kuingiza utulivu na uhakika duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma