

Lugha Nyingine
Mfumo wa kiikolojia wa kilimo wenye umri wa miaka 1,300 wang'aa katika Mkoa wa Yunnan, China (4)
KUNMING -Kilimo cha Mpunga, ufugaji samaki, na ufugaji bata -- vyote katika mashamba ya kwenye miteremko milimani. Njia hii ni ya maisha ambayo hutengeneza simulizi ya mapatano kati ya ikolojia, hekima ya jadi, na uvumbuzi wa kisasa.
Mandhari ya Kitamaduni ya Mashamba ya Mpunga kwenye Miteremko Milimani ya watu wa Kabila la Wahani katika eneo la Honghe, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China yaliorodheshwa kwenye Orodha ya Vitu vya Urithi wa Dunia ya UNESCO mwaka 2013. Mashamba hayo yanateremka kwenye miteremko mirefu ya Milima Ailao hadi kwenye kingo za Mto Honghe.
Katika kipindi cha miaka 1,300 iliyopita, watu wa Kabila la Wahani wameunda mfumo mkubwa wa mifereji ya kuleta maji kutoka kwenye vilele vya milima yenye misitu hadi kwenye mashamba hayo. Hii inaunda mfumo wa kiikolojia wa kilimo wa misitu, vijiji, mashamba na mito.
Kadiri mashamba hayo yalivyostawi, vivyo hivyo umaarufu wa mazao kama vile mchele mwekundu, samaki wa mashamba ya mpunga, na mayai ya bata. Sambamba na mvuto wa nyimbo za kale za Kabila la Wahani, mbinu za jadi za kilimo, na sherehe za kikabila, mashamba hayo yamekuwa yakivutia watalii kutoka kote duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma