China yashuhudia kuongezeka kwa safari za kurudi katika siku ya mwisho ya likizo ya Mei Mosi (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 06, 2025
China yashuhudia kuongezeka kwa safari za kurudi katika siku ya mwisho ya likizo ya Mei Mosi
Abiria wakiwa wameshuka treni kwenye Stesheni ya Reli ya Harbin mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China, Mei 5, 2025. (Picha na Yuan Yong/Xinhua)

Likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa China imechukua siku tano, kuanzia Mei Mosi hadi jana Jumatatu Mei 5, ambapo watu wamerudi kazini leo Jumanne, Mei 6. Katika siku hizo tano, Wachina wamekuwa wakisafiri sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kutembelea maeneo ya utalii, burudani, manunuzi na kufurahia kujumuika na familia.

Katika siku ya mwisho ya likizo hiyo, kilele cha safari nyingi za watu kurudi katika makaazi na maeneo yao ya kazi kimeshuhudia kote nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha