

Lugha Nyingine
China yaimarisha sera kuboresha usafiri na ununuzi kwa wageni wa kimataifa (2)
China ilianzisha kifurushi kipya cha hatua zinazolenga kurahisisha zaidi sera ya marejesho ya kodi wakati wa watalii kuondoka na kuongeza matumizi ya manunuzi kwa watalii wanaoingia China.
Hatua hizo, zilizotangazwa na Wizara ya Biashara ya China na idara zingine tano za serikali, zinajumuisha kupunguza kiwango cha chini zaidi cha ununuzi kwa marejesho ya kodi, kuongeza kikomo cha juu cha marejesho ya kodi kwa pesa taslimu, kutanua mtandao wa maduka yanayoshiriki na kupanua aina za bidhaa zinazopatikana.
Hatua hiyo ya hivi punde zaidi ya kuboresha sera ya marejesho ya kodi wakati wa watalii kuondoka inaimarisha mfululizo wa hatua ambazo China imeanzisha ili kurahisisha huduma za visa, malipo na malazi kwa watalii wa kimataifa, ikionyesha zaidi dhamira ya nchi hiyo ya kufungua mlango.
Sera za viza za China zimekuwa zikirekebishwa na kurahisishwa siku hadi siku. Kwa sasa, nchi hiyo imeruhusu uingiaji nchini humo wa bila visa kwa nchi 38, na imeongeza muda wa kuingia na kukaa China kwa kupita hadi saa 240 kwa wasafiri kutoka nchi 54. Mwaka 2024, uingiaji bila visa ulifikia safari milioni 20.12, ikiashiria ongezeko la asilimia 112.3 kuliko mwaka uliopita, kwa mujibu wa takwimu rasmi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma