Michezo ya Kimataifa ya MaJeshi Mwaka 2022 yamalizika nchini Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 29, 2022
Michezo ya Kimataifa ya MaJeshi Mwaka 2022 yamalizika nchini Russia
Timu ya China ikishiriki katika Michezo ya Kimataifa ya Majeshi Mwaka 2022 kwenye uwanja wa mazoezi ya kijeshi wa Alabino katika Eneo la Moscow, Russia, Agosti 27, 2022. Sherehe za kufunga Michezo ya Kimataifa ya Majeshi Mwaka 2022 zilifanyika kwenye uwanja wa kijeshi wa kizalendo huko Moscow, Russia Jumamosi. Fainali ya mbio za vifaru vya kivita ilifanyika kwenye uwanja wa mazoezi ya kijeshi wa Alabino Jumamosi mchana. Timu ya China imeshika nafasi ya pili katika mashindano haya. (Picha na Alexander Zemlianichenko Jr / Xinhua)

MOSCOW - Sherehe za kufunga Michezo ya Kimataifa ya Majeshi Mwaka 2022 zilifanyika kwenye uwanja wa kijeshi wa kizalendo huko Moscow, Russia Jumamosi.

Fainali ya mbio za vifaru vya kivita ilifanyika kwenye uwanja wa mazoezi ya kijeshi wa Alabino Jumamosi mchana. Timu ya China imeshika nafasi ya pili katika mashindano haya.

Michezo ya Kimataifa ya Majeshi Mwaka 2022 ilianza Agosti 13. Michezo hiyo ilifanyika katika maeneo ya nchi 12, zikiwemo China, Russia na Iran. Zaidi ya timu 270 kutoka nchi na maeneo 37 zilishiriki katika michezo hiyo.

Mwaka huu, Jeshi la China lilituma timu tisa nje ya nchi kushiriki katika mashindano nchini Russia, Iran, Kazakhstan, Algeria na Uzbekistan.

Michezo ya Kimataifa ya Majeshi, iliyoanzishwa na Wizara ya Ulinzi ya Russia, imekuwa ikitumika kama jukwaa la kimataifa la wanajeshi kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha