

Lugha Nyingine
Sao Tome na Principe yashinda vita dhidi ya Malaria chini ya msaada wa utaalamu wa matibabu wa China (3)
![]() |
Picha kutoka nyaraka iliyopigwa Julai 2, 2021 ikionesha kibanda cha kampeni ya usimamizi wa dawa za kiasi kikubwa (MDA) iliyotekelezwa na kundi la wataalam wa China katika vitongoji vya Sao Tome, Mji Mkuu wa Sao Tome na Principe. (Picha/Xinhua) |
Sao Tome na Principle iko njiani kutokomeza malaria chini ya msaada wa madaktari na matibabu ya China.
Nchi hii ya visiwa, ambayo idadi ya watu wake ni zaidi ya 200,000, imeathiriwa vibaya na malaria. Ilitoa ripoti ya watu 2,000 walioambukizwa malaria Mwaka 2020.
Nchi hiyo inajipanga kutokomeza ugonjwa huo ifikapo Mwaka 2025. “Bado tunahitaji juhudi kubwa ili kutimiza lengo hilo kwa kuwa kuna hali ya hewa yenye joto kali na unyevunyevu," Guo Wenfeng, Mshauri Mkuu wa kikundi cha wataalamu wa afya wa China nchini Sao Tome na Principle, aliliambia shirika la habari la China, Xinhua.
Kuanzia Mwezi Machi, mwaka huu, Bwana Guo na kikundi chake wameingia na kutoka mara kwa mara kwenye vijiji vya eneo la Agua-Grande ambapo hali ya kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu walioambukizwa malaria inaleta wasiwasi mkubwa, hivyo walianzisha kampeni kubwa ya matibabu dhidi ya malaria.
Kikundi hicho cha wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dawa za Mitishamba za China cha Guangzhou kimegundua njia bora—Artequick, dawa iliyotengenezwa kwa artemisinin, piperaquine na dozi ndogo ya primaquine.
Sehemu muhimu ya dawa hii, artemisinin, iligunduliwa na mwanasayansi wa China na mshindi wa Tuzo ya Nobel Tu Youyou kutoka artemisia annua.
Katika miaka iliyofuata, kwa msaada wa kikundi cha madaktari wa China, kiwango cha maambukizi ya malaria kimeripotiwa kushuka kutoka asilimia 60 hadi asilimia 3 katika miji midogo karibu na Mji Mkuu wa Sao Tome chini ya mradi wa matumizi ya kiasi kikubwa ya dawa (MDA).
Katika mji mdogo wa Liberdade, ambao ulikuwa moja ya maeneo yenye hali mbaya zaidi ya maambukizi ya malaria, hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa katika miezi minane mfululizo tangu yafanywe majaribio ya kutekeleza mkakati wa MDA mnamo Julai, 2019.
“Sisi wenyeji tunatumai kushirikiana na kikundi cha madaktari Wachina kukabiliana na malaria, kwa sababu tunataka kutokomeza ugonjwa huu hapa Liberdade na hatimaye Sao Tome na Principe,” anasema mkazi Vasco Guiva.
Mpango wa China “bila shaka umesadia kutimiza lengo la nchi hiyo la kutokomeza malaria ifikapo Mwaka 2025”, anasema Waziri wa Afya wa Sao Tome na Principe Filomena Monteiro, huku akisifu uungaji mkono wa China katika kazi hii ngumu.
Kwa Bwana Guo na kikundi chake , kazi bado inaendelea kwa kuwa kikundi cha wataalam wa China wataendelea kupambana na malaria nchini humo hadi ugonjwa huo utokomezwe .
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma