Mashambulizi ya droni yalenga Khartoum, miji mingine ya Sudan huku mapigano yakizidi kupamba moto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 14, 2026

Wazima moto wakipambana na moto baada ya shambulizi la droni kwenye kituo cha kuhifadhi mafuta, Port Sudan, mashariki mwa Sudan, Mei 6, 2025. (Wizara ya Utamaduni na Habari ya Sudan/kupitia Xinhua)

Wazima moto wakipambana na moto baada ya shambulizi la droni kwenye kituo cha kuhifadhi mafuta, Port Sudan, mashariki mwa Sudan, Mei 6, 2025. (Wizara ya Utamaduni na Habari ya Sudan/kupitia Xinhua)

KHARTOUM - Mashambulizi ya droni yaliendelea kote Sudan jana Alhamisi kwa siku ya pili mfululizo, yakilenga mji mkuu Khartoum na miji mingine kadhaa huku mapigano yakizidi kupamba moto kwenye maeneo mbalimbali ya mstari wa mbele katika Kordofan na Blue Nile.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka jeshini na mashuhuda, mashambulizi hayo yalilenga Khartoum, pamoja na El Obeid, mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Kaskazini; Kadugli, mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Kusini; na Atbara na Al-Damar katika Jimbo la Mto Nile, wakati huohuo ulinzi wa anga na mifumo ya ardhini ya ulinzi dhidi ya ndege ilikabiliana na wimbi jipya la droni.

Chanzo hicho kimesema droni zaidi ya 35, ambazo zinahusishwa na wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF), zilidondoshwa chini Jumatano wiki hii katika maeneo yakiwemo ya Atbara, Al-Damar na El Obeid.

Jeshi la Sudan halijatoa taarifa rasmi kuhusu mashambulizi hayo ya hivi punde, huku RSF haijatoa maoni yoyote juu ya madi hayo kwamba imehusika.

Sudan imekuwa ikikumbwa na mgogoro wa kivita kati ya SAF na RSF tangu katikati ya Aprili 2023, ambao umesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya watu kuhama makazi yao wa ndani na nje ya nchi.

Picha hii iliyopigwa Agosti 12, 2025 ikionyesha mwonekano wa ndani wa hospitali ya mafunzo iliyobomolewa katika migogoro kati ya Vikosi vya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Uungaji Mkono wa Haraka, Khartoum, Sudan. (Picha na Mohamed Khidir/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha