Lugha Nyingine
Wazambia wapiga kura katika uchaguzi mkuu huku amani ikitawala

Rais wa Zambia aliye madarakani Hakainde Hichilema akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura mjini Lusaka, Zambia, Agosti 13, 2026. (Picha na Martin Mbangweta/Xinhua)
LUSAKA - Wapiga kura wa Zambia walijitokeza kwa wingi jana Alhamisi kupiga kura zao katika uchaguzi mkuu huku kukiwa na mazingira ya amani kwa kiasi kikubwa.
Rais aliye madarakani sasa Hakainde Hichilema, ambaye anawania muhula wa pili, alipiga kura kwenye Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kabulonga mjini Lusaka, mji mkuu wa nchi hiyo, akitoa wito kwa wapiga kura kuendelea kuwa watulivu, kuonesha subira ya hali ya juu na kushirikiana na maafisa wa uchaguzi wakati wa mchakato wa kupiga kura.
Hichilema anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wagombea wengine 12, akiwemo Brian Mundubile, ambaye anagombea chini ya Chama cha Maridhiano ya Kitaifa kwa Umoja na Ustawi.
Zoezi la kupiga kura lilikuwa likitarajiwa kuisha saa 12:00 jioni kwa saa za Lusaka (16:00 GMT), baada ya hapo kazi ya kuhesabu kura ilikuwa imepangwa kuanza.
Kwa mujibu wa tume ya kusimamia uchaguzi ya Zambia, mgombea urais lazima apate asilimia zaidi ya 50 ya kura halali ili kushinda; vinginevyo, duru ya pili itafanyika.

Wapiga kura wakiwa wamepanga foleni ili kupiga kura zao katika kituo cha kupigia kura mjini Lusaka, Zambia, Agosti 13, 2026. (Picha na Martin Mbangweta/Xinhua)

Wapiga kura wakiwa wamepanga foleni ili kupiga kura zao katika kituo cha kupigia kura mjini Lusaka, Zambia, Agosti 13, 2026. (Picha na Martin Mbangweta/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



