Lugha Nyingine
China yazitaka nchi husika kuacha kutumia ovyoovyo mifumo ya kudhibiti silaha ya pande nyingi
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun amesema, kile kinachoitwa taarifa ya pamoja ya Marekani na nchi husika kwenye Mkutano wa Kupunguza Silaha kabisa kinatokana na kusudi la kisiasa, na ameongeza kuwa China inazihimiza nchi husika kuacha kutumia ovyoovyo mifumo ya kudhibiti silaha ya pande nyingi.
Vyombo vya habari vimetoa habari vikisema kuwa, kwenye Mkutano wa Kupunguza Silaha wa Agosti 11, Marekani na nchi husika zilitoa taarifa ya pamoja, zikidai kwamba shughuli za kufanya majaribio ya kurusha makombora zilizofanywa hivi karibuni kwenye eneo la Pasifiki hazikufuata “kitendo cha kigezo” cha kutoa taarifa kabla ya wakati, hali ambayo imeongeza hatari ya kufanya maamuzi kwa makosa na kudhoofisha utulivu katika eneo hilo, na nchi husika zinapaswa kutekeleza “Kanuni za Hague za Kuzuia Vitendo vya Uenezaji wa Makombora ya Balistiki”. Inaaminika kwamba taarifa hiyo ya pamoja inalenga majaribio ya kurusha makombora ya balistiki kwa nyambizi yaliyofanywa na China mwezi Julai mwaka huu.
Alipoulizwa maelezo yake baada ya habari jana Jumatano, msemaji Guo amesema kile kinachoitwa taarifa ya pamoja ya Marekani na nchi husika kwenye Mkutano huo wa Kupunguza Silaha, ambayo ikichukua kisingizio ya “Kanuni za Hague za kuzuia Uenezaji wa Makombora ya Balistiki” na kuashiria majaribio ya China ya kurusha makombora, kabisa inatokana na kusudi la kisiasa, na imefichua vya kutosha unafiki na undumilakuwili wao.
Msemaji huyo amesema, “China inazihimiza nchi husika kuacha kutumia ovyoovyo mifumo ya kudhibiti silaha ya pande nyingi, kutumia mazungumzo ya dhati badala ya mapambano yasiyo ya halali na kuweka masharti ya lazima kwa ajili ya kuimarisha mazungumzo na kubadilishana maoni katika eneo hilo la kudhibiti silaha,” Guo ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



