Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran asema kukidhi mahitaji ya afya ya Iran wakati wa vita ni kazi yenye changamoto ngumu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi akihudhuria hafla ambapo Wizara za Iran za Mambo ya Nje na ile ya Afya zinatia saini nyaraka ya makubaliano (MoU) juu ya ushirikiano katika kujenga upya miundombinu iliyobomolewa wakati wa vita mjini Tehran, Iran, Agosti 11, 2026. (Xinhua/Shadati)
TEHRAN - Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi amesema kwamba kukidhi mahitaji ya afya ya nchi hiyo ni miongoni mwa kazi yenye changamoto ngumu zaidi iliyofanywa na wizara yake wakati wa vita vya siku 40 na Marekani na Israeli.
Ametoa kauli hiyo jana Jumanne kwenye hafla iliyofanyika katika mji mkuu Tehran ya kusaini nyaraka ya makubaliano (MoU) kati ya Wizara za Mambo ya Nje na ile ya Afya za Iran juu ya ushirikiano katika kujenga upya miundombinu iliyobomolewa wakati wa vita hivyo, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Wanafunzi wa Iran.
Araghchi amesema Wizara ya Mambo ya Nje ilifanya kazi na Wizara ya Afya wakati wa vita ili kununua dawa na vifaa tiba na kuvisafirisha hadi nchini humo, akiielezea juhudi hiyo kuwa ni kazi yenye changamoto ngumu.
Februari 28, Israel na Marekani zilianzisha mashambulizi ya pamoja dhidi ya Tehran na miji mingine ya Iran, na kumuua Kiongozi Mkuu wa wakati huo Ali Khamenei na makamanda kadhaa wa kijeshi. Iran ilijibu kwa mfululizo wa mashambulizi ya makombora na droni ikiilenga Israeli na kambi na mali za Marekani katika eneo hilo.
Mwezi Juni, Iran na Marekani zilitia saini MoU juu ya kumaliza vita katika pande zote, ikiwa ni pamoja na Lebanon. Pande hizo mbili zilikuwa zimepangwa kufanya mazungumzo ndani ya kipindi cha siku 60 ili kufikia makubaliano ya mwisho, lakini kupamba moto kwa mizozo kwa hivi karibuni katika eneo hilo kumeacha hatma ya mazungumzo hayo bila uhakika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi akihudhuria hafla ambapo Wizara za Iran za Mambo ya Nje na ile ya Afya zinatia saini nyaraka ya makubaliano (MoU) juu ya ushirikiano katika kujenga upya miundombinu iliyobomolewa wakati wa vita mjini Tehran, Iran, Agosti 11, 2026. (Xinhua/Shadati)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi akihudhuria hafla ambapo Wizara za Iran za Mambo ya Nje na ile ya Afya zinatia saini nyaraka ya makubaliano (MoU) juu ya ushirikiano katika kujenga upya miundombinu iliyobomolewa wakati wa vita mjini Tehran, Iran, Agosti 11, 2026. (Xinhua/Shadati)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma