Lugha Nyingine
Machaguo ya Trump ya kujiondoa katika vita vya Iran yaripotiwa kupungua
WASHINGTON – Jarida la Wall Street limeripoti jana Jumapili kwamba mwenendo wa hivi karibuni katika mazungumzo unaonesha kuwa machaguo ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kujiondoa katika vita dhidi ya Iran "yamepungua."
Trump kwa wiki kadhaa "amekuwa akiweka msingi wa kutangaza ushindi katika vita vya Iran iwapo Tehran itafungua tena kabisa Mlango-Bahari wa Hormuz, na hata amependekeza wazo faraghani kwa wasaidizi wake waandamizi kwamba yuko tayari kujiondoa na vita hivyo bila makubaliano ya nyuklia," ripoti hiyo imerejelea maafisa wa Marekani wakisema.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa Trump alijaribu kujumuisha mazungumzo ya nyuklia kama sehemu ya mazungumzo mapana na Iran, "lakini hayo yamethibitika kuwa magumu sana, na kuifanya Ikulu ya White House katika wiki za hivi karibuni kujikita zaidi katika kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz."
Hata hivyo, "lengo hilo lililopunguzwa," limekuwa gumu zaidi wakati Iran iliposisitiza Jumamosi "kwa gharama yake ya juu zaidi" ya kutafuta mabilioni ya dola kutoka Marekani, kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka eneo hilo, na kukomeshwa kwa kizuizi cha majini cha Marekani, miongoni mwa mambo mengine, ripoti hiyo imesema, ikiongeza kuwa "machafuko ya hivi karibuni katika mazungumzo yameonyesha kuwa Tehran iko tayari kwa mgogoro wa muda mrefu na wenye kuchosha."
Ripoti hiyo ya hivi punde inakuja siku mbili baada ya CNN kuripoti kwamba Mwenyekiti wa Wakuu wa Majeshi ya Marekani, Jenerali Dan Caine, katika wiki chache zilizopita, amewaambia faragha washauri wengine waandamizi wa Trump na maafisa wa Baraza la Mawaziri kwamba Marekani inahitaji kupata njia ya kutoka kwenye vita hivyo na Iran.
Vyombo vya habari vimeripoti kwamba jeshi la Marekani lilikuwa limetumia karibu asilimia 80 ya makombora ya kuzuia kwa ajili ya mfumo muhimu wa ulinzi wa makombora wakati wa vita, huku makamanda wa kijeshi wakionya kwamba akiba ya silaha za jeshi iko ilikuwa "katika kiwango cha chini cha hatari."
Siku ya Alhamisi, Trump alikiri kwamba ingawa kwa ujumla akiba ya silaha ya Marekani inabaki ya kutosha, utoaji wa aina fulani za silaha ni "mdogo kwa kiasi fulani," bila kufafanua zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Gazeti la Washington Post siku ya Jumamosi, Pentagon inaitaka viwanda vya Marekani vya mambo ya ulinzi "kuongeza kasi ya uzalishaji na usafirishaji wa silaha," ikiwa ni pamoja na silaha ambazo "ziko katika uhaba mkubwa" kutokana na vita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



