Lugha Nyingine
Timu ya madaktari wa China yatoa huduma za bila malipo za afya kwa wagonjwa 700 nchini Tanzania
Kundi la 27 la Timu ya madaktari wa China nchini Tanzania imetoa huduma ya kliniki bila malipo kwa siku mbili katika mkoa wa Rukwa, magharibi mwa Tanzania, ikitoa huduma za afya kwa wakazi 700 wenyeji, na kuimarisha ushirikiano wa afya wa pande mbili.
Kliniki hiyo iliyofanyika Jumanne wiki hii chini ya mwongozo wa Ubalozi wa China nchini Tanzania na kwa mwaliko wa mamlaka za mkoa huo wa Rukwa, ilijikita katika kutoa huduma za afya kwa jamii zisizo na uwezo na watu wanaoishi maeneo ya pembezoni zaidi wanaoshindwa kupata huduma za afya.
Wataalamu wa magonjwa ya moyo, upasuaji wa moyo, mapafu na kifua, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, upasuaji wa jumla, na tiba ya mifupa walitoa huduma za kina, ikiwemo vipimo, utambuzi wa magonjwa, na mwongozo wa matumizi ya dawa.
Pia kliniki hiyo ilitoa matibabu ya magonjwa ya kawaida, na kutoa maelezo ya jinsi ya kudhibiti magonjwa sugu, na elimu ya afya kwa ujumla.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



