Makundi hasimu ya Sudan yatupiana lawama baada ya shambulizi la droni nchini Chad

(CRI Online) Machi 20, 2026

Makundi mawili hasimu nchini Sudan yametupiana lawama jana Alhamisi juu ya shambulizi la droni lililotokea katika mji wa Al-Tina nchini Chad, ambalo limesababisha vifo vya raia 17, huku Chad ikiapa kuwasaka wale waliotekeleza shambulio hilo.

Serikali ya Chad imethibitisha kuwa shambulizi hilo lilitokea Jumatano, na kwamba droni hiyo ilirushwa kutoka ndani ya ardhi ya Sudan.

Kundi la wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) la nchini Sudan limelaani kile lilichokiita kuwa ni shambulizi la droni, na kulilaumu Jeshi la Sudan (SAF), likilielezea kuwa ni “ukiukaji wa mamlaka huru ya Chad na uchocheaji hatari wa mvutano.”

Jeshi la Sudan limekanusha kuhusika na shambulizi hilo, pia limesema katika taarifa jana Alhamisi kuwa droni ya RSF ilishambulia mkusanyiko wa raia ndani ya Chad, likikielezea kitendo hicho kuwa sehemu ya “mtindo wa kujirudia” wa mashambulizi ya kuvuka mipaka.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha