Mtaalamu Mchina wa mpunga aleta mavuno mengi kwa wakulima wa Nigeria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 18, 2026

Fundi wa kilimo Mchina Yang Xiugang (wa kwanza, kulia) akichunguza athari za tabianchi ya eneo husika kwenye mazao mashambani katika Kijiji cha Zhouping cha Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Machi 10, 2026. (Xinhua/Yang Wenbin)

Fundi wa kilimo Mchina Yang Xiugang (wa kwanza, kulia) akichunguza athari za tabianchi ya eneo husika kwa mazao mashambani katika Kijiji cha Zhouping cha Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Machi 10, 2026. (Xinhua/Yang Wenbin)

GUIYANG - Katika siku za hivi karibuni, fundi Mchina wa kilimo Yang Xiugang amekuwa akipokea ujumbe kutoka kwa Muhammad Usman, mmoja wa wanafunzi wake nchini Nigeria, akiomba ushauri wa kilimo. Katika kipindi cha miaka iliyopita, amesaidia kuongeza mara tatu mavuno ya mpunga katika sehemu za nchi hiyo.

Yang anatoka Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China – kituo muhimu cha kitaifa cha uzalishaji wa mbegu za mpunga, chenye historia ya kuanzia mwaka 1976.

Utaalamu wa Yang katika sekta hiyo ulianza mwaka 1998 wakati naibu meneja mkuu wa kampuni ya mbegu ya wilaya hiyo alipofika katika sehemu ya asili yake ili kuendeleza uzalishaji wa mbegu. Yang alitumia fursa hiyo kujifunza mbinu za uzalishaji wa mbegu chotara za mpunga.

Baada ya kuwa mbobezi wa ujuzi huo, aliajiriwa na kampuni hiyo kuwa fundi. Katika miaka iliyofuata, alitumwa kwenye vitongoji kadhaa katika sehemu mbalimbali za wilaya hiyo ili kueneza uzalishaji wa mpunga chotara.

Mwaka 2013, kampuni hiyo ya mbegu ilishirikiana na Kampuni ya Mbegu ya Yuan katika Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, ambayo ilipanga kutuma mafundi nje ya nchi ili kueneza mpunga chotara. Yang akipendekezwa na kampuni yake, alianza jukumu lake la kuchangia teknolojia ya kilimo nje ya nchi.

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, jamaa huyo mwenye umri wa miaka 59 amefanya kazi katika nchi kadhaa, zikiwemo Bangladesh, Malaysia, Nigeria na Gambia. Ametengeneza aina za mpunga chotara zilizoboreshwa kulingana na mazingira ya nchi husika na kutoa mwongozo wa kiufundi kwa wakulima wenyeji.

Yang amekuwa akifanya kazi katika Jimbo la Jigawa, Nigeria, tangu mwanzoni mwa mwaka 2021.

"Hali ya hewa huko ni tofauti kabisa na ile ya China. Halijoto hubadilika kwa kasi sana kati ya mchana na usiku. Miche hukua haraka sana -- jani jipya kila baada ya siku tatu, ikilinganishwa na siku nne au tano kipindi hicho huko Cengong," amesema, akiongeza kuwa halijoto ya mchana nchini Nigeria inaweza kufikia nyuzi joto 38 hadi 39 Celsius, lakini usiku, hupungua hadi nyuzi joto 10 hadi 15 Celsius.

Akikabiliwa na hali hizi, Yang aliweka kando uzoefu wake nchini China na kuanza kutokea mwanzoni kuelewa mzunguko wa upandaji wa eneo hilo. Alitumia siku nyingi mashambani, akifuatilia kwa makini ukuaji wa mpunga na kurekodi halijoto, unyevunyevu, na ukuaji wa miche.

Baada ya miaka zaidi ya miwili ya utafiti, hatimaye ameielewa vema zaidi mifumo ya upandaji ya eneo hilo.

Shukrani kwa utaalamu wake, wastani wa mavuno ya mpunga umeongezeka kutoka kilo takriban 200 kwa mu (hekta karibu 0.067) mwaka 2021 hadi kati ya kilo 650 na 700 kwa mu ilipofikia mwaka 2025.

Hadi sasa, Yang amefunza wanafunzi 12 wenyeji nchini Nigeria, akiwemo Usman, ambaye amekuwa mkulima stadi.

Usman alianza kujifunza kutoka kwa Yang mwaka 2023. Anakumbuka kwamba mavuno ya mpunga katika aneo hilo yalikuwa ya chini na gharama za maisha zilikuwa juu.

"Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, nimejifunza hatua kwa hatua kilimo cha miche, udhibiti wa wadudu na ujuzi mwingine. Katika siku za baadaye, nitarithisha mbinu hizi za mpunga chotara ambazo nimejifunza kwa watu wengi zaidi." Usman amesema.

Mwezi ujao wa Aprili, Yang atarudi Nigeria. Anatarajia kupanua eneo la upandaji wa mpunga chotara wa eneo hilo hadi hekta 20,000 kabla ya kustaafu.

Fundi wa kilimo Mchina Yang Xiugang (wa pili kulia) akijifunza kuhusu uzalishaji wa mbegu za mpunga na mafundi wa kilimo wenyeji nyumbani kwa mwanakijiji katika Kijiji cha Zhuxi cha Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Machi 10, 2026. (Xinhua/Yang Wenbin)

Fundi Mchina wa kilimo Yang Xiugang (wa pili kulia) akijifunza kuhusu uzalishaji wa mbegu za mpunga na mafundi wa kilimo wenyeji nyumbani kwa mwanakijiji katika Kijiji cha Zhuxi cha Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Machi 10, 2026. (Xinhua/Yang Wenbin)

Fundi wa kilimo wa Mchina Yang Xiugang akichunguza ukuaji wa maua ya mbegu za rapa mashambani katika Kijiji cha Zhouping cha Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Machi 10, 2026. (Xinhua/Yang Wenbin)

Fundi wa kilimo wa Mchina Yang Xiugang akichunguza ukuaji wa maua ya mbegu za rapa mashambani katika Kijiji cha Zhouping cha Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Machi 10, 2026. (Xinhua/Yang Wenbin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha