

Lugha Nyingine
China inayofungua mlango, fursa za pamoja
Mwaka 2024, uagizaji matunda kutoka nchi za ASEAN kupitia Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China ulifikia kiwango cha juu cha tani karibu milioni 2.5.
Ukiwa ni kituo cha kwanza na kitovu kikuu cha matunda ya ASEAN kuingia soko la China, mkoa huo wa Guangxi unageuza maono ya "Kuzalishwa ASEAN, kusambazwa mkoani Guangxi, na Kuuzwa China" kuwa uhalisia. Mtindo wa biashara wa "kununua kutoka ASEAN, kuuza kote nchini; kununua kote nchini, kuuza ASEAN" unazidi kuwa halisi.
Katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, mji wa Shenzhen, mji wa kisasa wa kimataifa, na Shanwei, kituo cha zamani cha mapinduzi kinachohitaji maendeleo, viko umbali wa kilomita zaidi ya 100 kati yao. Ukienea kutoka Shenzhen hadi Shanwei, "ushoroba wa dhahabu" wa viwanda vya magari yanayotumia nishati mpya (NEV) umeundwa. Kampuni za kiviwanda takriban 30 za uzalishaji wa awali na wa mwisho zimeunganishwa kama viungo kwenye myororo, zikiunda kundi la viwanda vya NEV lenye thamani ya mamia ya mabilioni ya yuan.
Kupitia Bandari ya Kimataifa ya Uchukuzi ya Xiaomo, ambayo inajenga mafungamano kati ya bandari na viwanda, mauzo ya nje ya China ya NEV yanapata msukumo mkubwa na kuharakisha upanuzi wao katika masoko ya kimataifa.
Ndani ya muda wa saa nane na nusu tu, kaa freshi wa Norway wanaweza kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zhengzhou Xinzheng katika Mkoa wa Henan, katikati mwa China, wakiwa bado wamefunikwa na maji ya bahari katika nyuzi joto za hasi mbili. Kutokana na "Njia ya Hariri ya Angani" ya Zhengzhou-Luxembourg, vyakula vitamu vya Ulaya sasa vinaweza kufika China ndani ya siku moja.
China inafanya juhudi madhubuti kujenga mfumo mpya kwa uchumi uliofungua mlango kwa kiwango cha juu zaidi, huku ufunguaji mlango ukiwa ni sifa maalum ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China. Idadi ya vipengele kwenye orodha hasi ya uwekezaji wa kigeni imeendelea kupungua. Vizuizi vyote katika sekta ya viwanda vimeondolewa, na mipango ya majaribio ya kufungua sekta za huduma kama vile huduma ya mawasiliano ya simu yenye thamani iiliyoongezwa na teknolojia ya baiolojia inaendelea hatua kwa hatua.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, China imekuwa ikipanua kiwango cha kufungua mlango, huku mfululizo wa mipango mikuu ikitolewa ili kunufaishana fursa na kutafuta maendeleo na nchi nyingine duniani. Licha ya hali ya kutokuwa na uhakika katika mazingira ya kimataifa, China inabaki kuwa nchi inayotoa mchango mkubwa zaidi katika ukuaji wa uchumi duniani na nguzo ya kutuliza uchumi wa dunia.
Misri yafunga Jumba la Makumbusho Kuu la Misri kwa ajili ya kufunguliwa rasmi
Mwezi mpevu wavutia kote China wakati wa Sikukuu ya Mbalamwezi ya China
Wanasarakasi wafanya maonyesho katika Eneo la Ulimwengu wa Sarakasi la Wuqiao mjini Cangzhou, China
Sikukuu ya mavuno ya wakulima yaadhimishwa katika Mkoa wa Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma