Uganda, DRC zakubaliana kufanya doria za pamoja katika Ziwa Edward kufuatia shambulizi kubwa

(CRI Online) Oktoba 17, 2025

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimekubaliana kuimarisha operesheni za pamoja za kiusalama kwenye eneo la Ziwa Edward baada ya kutokea kwa shambulizi kubwa lililofanywa na watu wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa Kongo.

Msemaji wa Jeshi la Uganda (UPDF) Kiconco Tabaro amesema kwenye taarifa iliyotolewa Jumatano wiki hii kuwa makamanda wa UPDF na Jeshi la DRC (FARDC) wamekutana katika Bandari ya Kasindi katika eneo la Beni la DRC, kwa nia ya kuimarisha uratibu wa jeshi la majini na mifumo ya usalama kando ya Ziwa Edward.

Aidha, wamekubaliana kuchukua hatua za kuhimiza ushirikiano ikiwemo kufanya doria za pamoja kwenye Ziwa hilo, kufanya mikutano ya uratibu wa mambo ya usalama na uvuvi kila baada ya muda, na kuelimisha jamii ya wavuvi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha