Rais wa Angola amsema, Angola itaenzi safari ya kihistoria wakati wa kuadhimisha miaka 50 tangu kupata uhuru

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 17, 2025

Wabunge wa Bunge la Taifa la Angola wakihudhuria ufunguzi wa mwaka mpya wa bunge mjini Luanda, Angola, Oktoba 15, 2025. (Picha na Julio Kikebu/Xinhua)

Wabunge wa Bunge la Taifa la Angola wakihudhuria ufunguzi wa mwaka mpya wa bunge mjini Luanda, Angola, Oktoba 15, 2025. (Picha na Julio Kikebu/Xinhua)

LUANDA - Rais wa Angola Joao Lourenco amesema kuwa sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu nchi hiyo kupata uhuru zitakuwa "tukio la kuenzi safari ya kihistoria ya Angola, kupitia upya mafanikio na changamoto."

Akitoa hotuba ya Hali ya Taifa siku ya Jumatano kwenye ufunguzi wa mwaka mpya wa bunge, Lourenco amesema kuwa Novemba 11, watu wa Angola wataadhimisha miaka 50 tangu nchi hiyo ipate uhuru, miaka 50 wakiwa watu huru, mabwana wa mustakabali wao wenyewe.

Siku hiyo itakuwa wakati wa kuheshimu "nyakati nzuri na zisizo nzuri za historia yetu, mafunzo tuliyojifunza na ushindi tuliopata pamoja," amesema.

Angola, ambayo wakati fulani iliibuka kutoka "usiku mrefu wa ukoloni," imebadilika sana katika miongo mitano iliyopita, Rais Lourenco amesema.

"Kutoka kwa wakazi wapatao milioni 6.5 mwaka 1975, Angola leo ina watu takriban milioni 35," amesema, akiongeza kuwa ukuaji wa kasi wa watu unaleta changamoto katika kutoa huduma za afya, elimu, makazi na huduma za kijamii.

Rais Lourenco amekumbushia kuwa wakati wa uhuru, Angola ilikuwa na vituo vya afya 320 tu na madaktari 19, lakini sasa ina vituo vya afya 3,355, na idadi ya vifo vya watoto wachanga na wajawazito imepungua kwa kiasi kikubwa.

"Wastani wa umri wa watu kuishi umeongezeka hadi miaka 64.6, ikimaanisha kwamba Waangola wanaishi kwa wastani wa miaka 23 zaidi kuliko mwisho wa kipindi cha ukoloni," amesema.

Katika sekta ya elimu, rais huyo amesema, Angola ilirithi mfumo wa kikoloni na usio na usawa wenye kiwango cha kutojua kusoma na kuandika cha asilimia 85, ambacho sasa kimeshuka hadi asilimia takriban 24.

Kuhusu uchumi, Rais Lourenco amesema serikali inajaribu kudhibiti mfumuko wa bei, ambao unasimama karibu asilimia 18, na kuimarisha ujumuishaji wa kifedha, ikilenga kiwango cha huduma za benki cha asilimia 65 ifikapo mwaka 2027.

Amesisitiza tena hitaji la kuwa na uchumi wa sekta mbalimbali, akirejelea maneno ya rais mwasisi Agostinho Neto kwamba "kilimo ni msingi na viwanda ni jambo kuu."

Rais Joao Lourenco wa Angola akitoa hotuba ya Hali ya Taifa katika ufunguzi wa mwaka mpya wa bunge mjini Luanda, Angola, Oktoba 15, 2025. (Picha na Julio Kikebu/Xinhua)

Rais Joao Lourenco wa Angola akitoa hotuba ya Hali ya Taifa katika ufunguzi wa mwaka mpya wa bunge mjini Luanda, Angola, Oktoba 15, 2025. (Picha na Julio Kikebu/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha