

Lugha Nyingine
China kuboresha udhibiti wa uuzaji nje wa madini adimu, kuwezesha biashara halali
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China, He Yongqian amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Alhamisi kwamba China itakuwa ikiendelea kurahisisha taratibu za utoaji leseni na kupunguza muda wa mapitio katika kutekeleza udhibiti wake wa hivi karibuni wa uuzaji nje wa madini adimu, na itazingatia kikamilifu hatua za uwezeshaji ili kuhimiza biashara halali kwa ufanisi.
"Hatua hizo zilizotolewa hivi karibuni za udhibiti wa uuzaji nje ni juhudi za kawaida ambazo serikali ya China imefanya kuboresha mfumo wa udhibiti wa uuzaji nje wa China kwa mujibu wa sheria na kanuni, na hazilengi nchi au eneo lolote mahsusi," msemaji huyo wa wizara amesema.
"Maombi yote ya kuuza nje yanayokidhi taratibu kwa matumizi ya kiraia yatapitishwa," amesema.
Amesema kuwa udhibiti huo unajumuisha utendaji halali ulioundwa kuzuia matumizi haramu ya madini adimu, kama vile matumizi katika silaha za maangamizi makubwa, hivyo kulinda usalama wa taifa la China na usalama wa pamoja duniani.
"China ilikuwa imeziarifu nchi na maeneo husika kabla ya kutangaza hatua hizi za udhibiti wa uuzaji nje, na sasa iko katika mawasiliano na pande husika kuhusu uwezeshaji wao," msemaji huyo amesisitiza.
Amesema kwamba China inaeleza kutoridhika kwake na upingaji mkali kwa mfululizo wa hatua za vizuizi ambazo Marekani imechukua, zikiwemo tangazo lake la hivi karibuni la sheria mpya ambayo inapanua vizuizi vyake vya "orodha ya vitu", vya kuuzwa nje vilevile hatua ya kuweka ada za ziada za bandari kwa meli za China kufuatia uchunguzi wa Kifungu cha 301.
"China inaitaka Marekani kurekebisha mara moja kitendo chake hicho potovu," ameongeza.
Amesema kuwa uchunguzi wa Kifungu cha 301 na hatua za vizuizi zinazolenga sekta ya uundaji wa meli ya China, miongoni mwa viwanda vingine, ni mifano halisi ya utekelezaji wa uamuzi wa upande mmoja na kujihami.
"Hatua hizi si tu zitaharibu maslahi ya viwanda husika vya China, lakini pia zitaongeza mfumuko wa bei wa ndani nchini Marekani, kudhoofisha ushindani wa bandari za Marekani na kuathiri ajira za Marekani," amesema.
Hatua hizo zimevuruga utulivu wa minyororo ya usambazaji duniani na kuleta machafuko katika sekta ya kimataifa ya usafiri wa meli, amesema, akisisitiza kwamba hatua zinazolingana za China ni hatua za kujilinda zilizochukuliwa kwa umuhimu na zinalenga kulinda uwanja sawa katika masoko ya usafiri wa meli na uundaji wa meli duniani.
Amesema baada ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara ya Madrid kati ya China na Marekani, upande wa Marekani, ukipuuza maneno ya China ya kupinga ya mara kwa mara, ulianzisha hatua 20 za kuikandamiza China katika muda wa siku 20 tu, ikiharibu vibaya maslahi ya China na kuvuruga mazingira ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili.
Amesema kuwa China hairidhiki sana na mfululizo wa hatua hizo zinazochukuliwa na upande wa Marekani na inazipinga vikali.
Misri yafunga Jumba la Makumbusho Kuu la Misri kwa ajili ya kufunguliwa rasmi
Mwezi mpevu wavutia kote China wakati wa Sikukuu ya Mbalamwezi ya China
Wanasarakasi wafanya maonyesho katika Eneo la Ulimwengu wa Sarakasi la Wuqiao mjini Cangzhou, China
Sikukuu ya mavuno ya wakulima yaadhimishwa katika Mkoa wa Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma