Rais Xi Jinping aipongeza FAO kwa kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 17, 2025

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amelipongeza Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake. Katika salamu zake za pongezi za jana Alhamisi, Rais Xi amesema kuwa shirika la FAO limekuwa likibeba jukumu muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula duniani, kuhimiza maendeleo ya vijiji, kufanyia mageuzi mifumo ya chakula, na kuboresha viwango vya maisha ya watu katika nchi mbalimbali.

Rais Xi amesisitiza kuwa, serikali ya China inaweka umuhimu mkubwa katika usalama wa chakula, na inashikilia kujitegemea yenyewe ili kuhakikisha utoaji wa chakula kwa watu wake zaidi ya bilioni 1.4, na pia kutoa msaada kwa iwezavyo kwa nchi zinazohitaji, ikichangia katika kulinda usalama wa chakula duniani.

Rais Xi amesema, "China, kama inavyofanya siku zote, itaiunga mkono FAO katika kubeba jukumu muhimu katika sekta ya chakula na kilimo duniani.” Na ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, kusukuma mbele Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kutoa mchango mpya na mkubwa zaidi kwa ajili ya kuboresha ustawi wa watu wa nchi zote.

Shirika la FAO lilianzishwa Oktoba 16, 1945, na China ni moja ya nchi wanachama waanzilishi wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha