Mfumuko mkuu wa bei wa China waongezeka kwa miezi 19, ikiashiria kuongezeka zaidi kwa mahitaji ya ndani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2025

BEIJING - Bei za wanunuzi za China zilionyesha dalili zaidi za utulivu mwezi Septemba, huku mfumuko mkuu wa bei ukifikia kiwango chake cha juu zaidi katika miezi 19, ikidhihirisha kuimarika kwa madhubuti katika mahitaji ya ndani, takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) jana Jumatano zinaonesha.

Takwimu hizo, zinaonyesha kuwa kiwango cha bei ya mlaji (CPI) cha China, ambacho hakijumuishi bei ya chakula na nishati, kilipanda kwa asilimia 1 kuliko mwaka jana wakati kama huo -- kikiashiria mwezi wa tano mfululizo wa kuongezeka na ongezeko kubwa zaidi tangu Februari 2024.

Hasa, takwimu hizo zinaonyesha kuwa bei ya vito vya dhahabu ilipanda kwa asilimia 42.1 kutoka mwaka mmoja uliopita, vifaa na vitu vya matumizi ya nyumbani vinavyotumia umeme bei zake ziliongezeka kwa asilimia 5.5, na vifaa vya mawasiliano bei zake ziliongezeka kwa asilimia 1.5. Gharama za matibabu na huduma za nyumbani zilipanda kwa asilimia 1.9 na asilimia 1.6, mtawalia.

CPI kuu pia ilionyesha mwelekeo chanya – ikirekodi ongezeko la asilimia 0.1 kuliko mwezi uliopita kutoka rekodi ya Agosti isiyobadilika na kupunguza kushuka kwake kwa mwaka hadi asilimia 0.3 -- ikilinganishwa na kushuka kwa mwaka kwa asilimia 0.4 mwezi Agosti, kwa mujibu wa takwimu hizo za NBS.

Mtakwimu wa NBS Dong Lijuan amehusisha kupungua huko kuliko mwaka jana wakati kama huo kwa CPI kuu hasa na "athari za msingi" kutoka mwaka jana, akisisitiza kuwa ushawishi huo kutoka kwenye mabadiliko ya bei ya mwaka huu umekuwa mzuri.

"Soko la wanunuzi lilibakia kuwa tulivu mwezi Septemba," Dong amesema.

Amesema ishara hizi za kutia moyo katika bei za wanunuzi zinaonyesha mahitaji ya ndani yanaendelea kufufuka, kukisababishwa na hatua nyingi za kuunga mkono matumizi zilizoletwa mwaka huu.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, mpango wa ruzuku kwa "kubadilisha bidhaa za zamani kwa kununua bidhaa mpya", moja ya mipango mikubwa nchini humu, umeonekana kuwa na ufanisi mkubwa ambapo kuanzia Januari hadi Agosti, wanunuzi milioni 330 walidai ruzuku hiyo, ikichochea yuan zaidi ya trilioni 2 (dola za Kimarekani zaidi ya bilioni 280) za mauzo ya bidhaa husika kuanzia simu janja na vifaa vya nyumbani vya umeme hadi baiskeli za umeme nchini kote.

China hivi karibuni ilitenga yuan nyingine bilioni 69 kwa serikali za mitaa kufadhili biashara ya wanunuzi "kubadilisha bidhaa za zamani kwa kununua mpya", ikisababisha ufadhili wa mwaka mzima wa serikali kuu wa yuan bilioni 300 kulipwa kikamilifu.

Mbali na matumizi ya bidhaa, matumizi ya huduma pia yameongezeka. Msemaji wa NBS Fu Linghui amesema kuwa mahitaji makubwa ya shughuli za usafiri na burudani yameendelea kuchochea matumizi ya huduma mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha