

Lugha Nyingine
Kuchangia Nguvu ya China katika Maendeleo ya Mambo ya Wanawake Duniani
Wanawake ni nguvu muhimu ya kusukuma mbele maendeleo ya jamii ya binadamu. Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikihimiza maendeleo ya sifa bora ya mambo ya wanawake nchini humu, siku zote inafanya juhudi za kujenga mazingira ya kimataifa yanayosaidia maendeleo ya wanawake, na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya mambo ya wanawake duniani.
Kwa kupitia utoaji msaada wa mradi wa Juncao na mafunzo ya ufundi duniani kote, upande wa China umesaidia wanawake wa zaidi ya nchi 100 kupata nafasi za ajira. Lin Dongmei, binti wa Lin Zhanxi anayesifiwa kuwa "Baba wa Juncao", alikwenda mara kwa mara barani Afrika na Oceania, ili kuwafundisha wanawake huko ana kwa ana ufundi wa kazi ya kupanda Juncao. Kutoka kutekeleza miradi ya ustawi wa maisha ya watu ikiwemo "mradi wa afya ya wanawake na watoto wa kike" na "mradi wa shule yenye furaha", hadi kutumia mfuko wa maendeleo ya dunia na ushirikiano wa Kusini-Kusini kwa kuanzisha miradi ya wanawake katika zaidi ya nchi 20......Upande wa China kwa kupitia mfululizo wa hatua za kivitendo umekuwa ukisaidia nchi zinazoendelea kuboresha mazingira kwa maisha na maendeleo ya wanawake, na kuwaunga mkono kutimiza lengo la kujitegemea na kujiendeleza.
Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikiendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika ujenzi wa uwezo wa wanawake, na kuanzisha mfumo wa mafunzo wa ngazi mbalimbali na unaofikia maeneo mengi. Imeanzisha Kituo cha Mafunzo cha Ushirikiano na Mawasiliano na Maendeleo ya Wanawake wa Dunia, ambacho kimeandaa miradi mbalimbali ya kuwapa uwezo wanawake; Imeanzisha vituo vya mafunzo (au mawasiliano) vya wanawake kwa kushirikiana na nchi nyingine 15, na kutoa mafunzo katika darasa la karakana badala ya vyumba vya mkutano. Mafunzo yaliyoandaliwa na China si kama tu yanahusu mafunzo ya ufundi wa kazi, bali pia yamewajengea wanawake wa nchi zinazoendelea njia ya "kujitegemea kwa ufundi."
China ikiwa mtekelezaji mwenye juhudi wa Azimio la 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Wanawake, Amani na Usalama, siku zote inaunga mkono wanawake kushiriki katika kuzuia migongano, kufanya mazungumzo ya amani na kujenga upya maskani. Tangu China ilipotuma kikosi chake cha kwanza cha walinda amani nchini Lebanon mwaka 2006, vikundi vya walinzi wanawake wa China vimekuwa vikienda mstari wa mbele katika medani. Mnamo mwaka 2020, katika Siku ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa, ofisa mwanamke wa kijeshi wa China aliyekuwa Lebanon, Xin Yuan, alipewa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Mtetezi wa Usawa wa Jinsia katika mambo ya kijeshi. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kikosi cha matibabu cha walinda amani wa China kilifanya ushirikiano na Kijiji cha Watoto cha SOS cha Kimataifa mjini Bukavu, ambapo wanajeshi wanawake wa China wanajulikana kama "China Mama." China imekuwa na zaidi ya wanajeshi wanawake 1,200 na zaidi ya askari polisi wanawake 100 waliotumwa katika operesheni za ulinzi wa amani. Aidha, Mfuko wa Amani na Maendeleo wa China–Umoja wa Mataifa umeanzisha mradi maalum wa mafunzo kwa wanawake wa daraja la juu, ili kuwaandaa makamanda wanawake kwa ajili ya shughuli za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.
Kutoka utoaji msaada wa ufundi wa kazi hadi utoaji mafunzo ya uwezo, kutoka miradi ya kuwapa uwezo wanawake hadi kukabiliana kwa pamoja na changamoto za kimataifa, China siku zote inafanya juhudi kwa vitendo halisi na kwa uwazi katika kusukuma mbele maendeleo ya mambo ya wanawake duniani, ikipunguza pengo la maendeleo kati ya wanawake wa nchi mbalimbali. Katika siku za baadaye, China itaendelea kushirikiana na pande mbalimbali kwa kuhimiza maendeleo endelevu ya wanawake duniani yanayowashirikisha watu wengi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma