

Lugha Nyingine
Watatu washinda Tuzo ya Nobel ya Kemia kwa kuunda mifumokazi ya kioganiki ya metali
Tuzo ya Nobel ya Kemia ya 2025 ikitangazwa Stockholm, Sweden, Oktoba 8, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)
STOCKHOLM - Susumu Kitagawa, Richard Robson na Omar M. Yaghi wametunukiwa Tuzo ya Nobel ya Kemia ya mwaka 2025 jana Jumatano kwa kuunda mifumo ya kioganiki ya metali (MOFs), Taasisi ya Sayansi ya Kifalme ya Sweden imetangaza.
"Washindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia 2025 wameunda miundo ya molekuli yenye nafasi kubwa kupitia kwayo gesi na kemikali nyingine zinaweza kutiririka," taasisi hiyo imesema katika taarifa.
Imeongeza kuwa miundo hiyo, mifumokazi ya metali-kioganiki, inaweza kutumika kwa kuvuna maji kutoka hewa ya jangwa, kunasa kaboni dioksidi, kuhifadhi gesi zenye sumu au kuchochea matokeo ya mchanganiko wa kikemikali.
Kitagawa ni profesa katika Chuo Kikuu cha Kyoto nchini Japani. Robson, mzaliwa wa Uingereza, anafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Melbourne nchini Australia. Yaghi, mzaliwa wa Amman, Jordan, ni profesa katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley nchini Marekani.
"MOFs zina uwezo bora mkubwa, kuleta fursa ambazo hazikuonekana hapo awali kwa kutengeneza mahsusi nyenzo zenye uwezo mpya," amesema Heiner Linke, mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Nobel ya Kemia.
Tuzo ya Nobel ya Kemia ya 2025 ikitangazwa Stockholm, Sweden, Oktoba 8, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma