Kituo cha Huduma za Mtandaoni cha Biashara ya Kimataifa cha Shenzhen Qianhai: Kusaidia Kampuni za China Kustawi katika Masoko ya Ng'ambo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2025

"Kama ukitaka kwenda kimataifa, tafuta Qianhai. Ukitaka kwenda kimataifa, nenda Qianhai." Kikiwa ni chombo muhimu cha ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa eneo la Qianhai, Shenzhen, Kituo cha Huduma za Mtandaoni (e-station) cha Biashara ya Kimataifa cha Shenzhen Qianhai ni jukwaa linalojumuisha huduma za mtandaoni na nje ya mtandaoni kwa kampuni za Mji wa Shenzhen, China zinazotaka kujitanua ng'ambo, ambalo liliundwa kwa pamoja na Mamlaka ya Qianhai na idara nyingine 32, ikiwemo Idara ya Biashara ya Mji wa Shenzhen.

He Yang, mkuu wa Kituo cha Huduma za Mtandaoni cha Biashara ya Kimataifa cha Shenzhen Qianhai na mkurugenzi mtendaji na meneja mkuu wa Kampuni ya Mambo ya Katibu ya Kibiashara ya Qianhai mjini Shenzhen amesema katika mahojiano na People's Daily Online jana Jumatatu kwamba, jukwaa hilo limedhamiria kuzipa kampuni za China huduma jumuishi, zote katika sehemu moja, kwa ajili ya kwenda kimataifa, na limetimiza mnyororo kamili, usanidi kamili, mchakato kamili wa huduma, na ufikiaji wa kina.

Amesema, kituo hicho kimeleta pamoja mashirika zaidi ya 200 ya huduma za kitaalamu na kusukuma uundaji wa "Shirikisho la Huduma za Kampuni kwenda Kimataifa," linalojumuisha sekta muhimu kama vile sheria, dawa na vifaa tiba, na tamthilia fupi. Linatoa huduma 70 za umma na limeanzisha kanda 10 za huduma maalum. Limehudumia kampuni zaidi ya 600 zinazoenda kimataifa, likiwa na watumiaji 15,000 waliosajiliwa mtandaoni na watembeleaji zaidi ya 360,000 wa jukwaa.

He Yang amesema kuwa jukwaa hilo litaendelea kuboresha huduma zake, likipanuka kutoka Qianhai na kwenda kote China ili kusaidia kampuni nyingi zaidi kwenda kimataifa kwa utaratibu, ufanisi na usalama, na kuziwezesha kufikia ukuaji thabiti na kupata mafanikio ya muda mrefu katika masoko ya nje ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha