

Lugha Nyingine
Mashindano ya michezo yanayofadhiliwa na China yaweka njia kwa vijana wa Afrika kuelekea jukwaa la kimataifa
Mashindano ya michezo ya simu ya mkononi ya Afrika ambayo yanashirikisha timu 16 kutoka bara hilo yamemalizika Jumapili huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ambapo timu kutoka Afrika Kusini ilipata ubingwa.
Fainali za Mashindano ya Michezo ya Simu za Mkononi ya PUBG (PMAC) ya Mwaka 2025 zilizofanyika kwa siku mbili ziliandaliwa na Kampuni ya Teknolojia ya China, Tencent, pamoja na Shirikisho la Michezo ya Kielektroniki (Esports) la Kenya, na Kampuni ya Simu ya China, Infinix.
Mkuu wa Kampuni ya Michezo ya Simu za Mkononi ya PUBG ya Afrika Brian Gu amesema lengo la mashindano hayo ni kuinua hadhi ya wachezaji wa michezo ya kielektroniki wanaotoka Afrika katika jukwaa la kimataifa.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Kielektroniki la Kenya Ronny Lusigi amesema fainali za PMAC 2025 ziliwasajili watu zaidi ya 10,000, ambayo ni rekodi mpya katika historia ya mashindano hayo barani Afrika. Ameongeza kuwa tukio hili limeonesha umuhimu unaokua wa michezo barani Afrika, ambapo Kenya yenyewe ina wachezaji wapatao 300,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma