Rais mstaafu wa Sao Tome na Principe: Ushindi wa vita ya China dhidi ya uvamizi wa Japan ulichochea uhuru wa nchi za Afrika

(CRI Online) Septemba 16, 2025

Manuel Pinto da Costa, former president of Sao Tome and Principe, is pictured during an interview with Xinhua on Aug. 19, 2025. (Xinhua/Liu Jie)

Manuel Pinto da Costa akihojiwa na Xinhua Agosti 19, 2025. (Xinhua/Liu Jie)

Aliyekuwa rais wa Sao Tome na Principe, Manuel Pinto da Costa amesema, vita ya watu wa China dhidi ya uvamizi wa Japan ilichochea kwa kiasi kikubwa mapambano ya kudai uhuru katika nchi za Afrika.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Pinto da Costa amesema ushindi wa China katika vita hiyo sio tu ulibadili mandhari ya kimataifa, bali pia ulijenga msingi wa urafiki kati ya Afrika na China katika njia ya kutafuta uhuru na maendeleo ya kitaifa ya nchi za bara hilo.

Amesema ushindi wa China umeionyesha dunia kuwa pale watu wakitamani uhuru na ukombozi, hakuna nguvu inayoweza kuwazuia, na ushindi huo uliwaaminisha Waafrika kwamba, alimradi wanasimama kwa pamoja, uhuru na ukombozi ni mambo yanayowezekana kupatikana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha