

Lugha Nyingine
China yasema uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Huangyan hauruhusiwi kuingiliwa kati
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesisitiza kuwa, Kisiwa cha Huangyan ni eneo la asili la China, na uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa ya Huangyan ni jambo la ndani ya mamlaka ya China ambalo lina uhalali wa kisheria, na haliruhusiwi kuingiliwa kati.
Lin Jian amesema hayo kufuatia kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bw. Marco Rubio, kwamba Marekani inasimama pamoja na mshirika wake Ufilipino, kupinga hatua ya China kuanzisha hifadhi ya taifa huko Kisiwa cha Huangyan.
Bw. Lin pia amesema China itaendelea kushirikiana na nchi za Jumuiya ya ASEAN kutekeleza kikamilifu Azimio la Utekelezaji la Wahusika wa Bahari ya Kusini ya China, na kuhimiza majadiliano ya kanuni na vitendo kwenye eneo la Bahari ya Kusini, ili kuijenga kwa pamoja Bahari hiyo kuwa ya amani, urafiki na ushirikiano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma