

Lugha Nyingine
Qatar yasema itaendelea na juhudi za upatanishi kuhusu mgogoro wa Gaza
Waziri Mkuu wa Qatar na waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani, amesema Qatar itaendelea na juhudi za usuluhishi ili kusimamisha mapambano katika Ukanda wa Gaza.
Kwenye mkutano wa maandalizi kwa mkutano wa kilele wa dharura kati ya nchi za Kiarabu na za Kiislamu, Bw. Mohammed amesema mashambulizi ya Israel dhidi ya Qatar hayataizuia Qatar kuendelea kushirikiana na Misri na Marekani kwa ajili ya upatanishi kuhusu mgogoro wa Gaza. Amesema kama watu wa Palestina hawawezi kutimiza haki zao halali, basi eneo hilo halitaweza kutimiza usalama na amani. Ameongeza kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Qatar ni ugaidi wa kitaifa, na ni kitendo ambacho kimekiuka sheria ya kimataifa na kanuni za kidiplomasia na kimaadili.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu na za Kiislamu walioshiriki kwenye mkutano huo, wamesema usalama wa Qatar ni sehemu isiyotengeka kwa usalama wa nchi za Kiarabu na za Kiislamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma