

Lugha Nyingine
Rais Xi asisitiza kujenga soko kuu la nchi nzima na kuhimiza maendeleo bora ya uchumi wa baharini
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) jana Jumanne katika mkutano wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya Kamati Kuu ya Chama ambayo anaiongoza, amesisitiza juhudi za kuendeleza ujenzi wa soko kuu la nchi nzima la mfumo wa sheria na kanuni za pamoja na kuhimiza maendeleo bora ya hali ya juu ya uchumi wa baharini.
Katika hotuba yake kwenye mkutano huo, Rais Xi amesisitiza kwamba kujenga soko kuu la nchi nzima la mfumo wa sheria na kanuni za pamoja ni muhimu kwa kuanzisha muundo mpya wa maendeleo na kuhimiza maendeleo bora ya hali ya juu, ni lazima kuimarishwa kwa uratibu na ushirikiano ili kukusanya nguvu za pamoja za kazi husika.
Rais Xi amesisitiza kwamba kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China ni lazima kuhimiza maendeleo bora ya hali ya juu ya uchumi wa baharini ili kufuata njia ya China ya kutumia rasilimali za baharini kwa kuimarisha nchi yenye nguvu. Mkutano huo umesema kuwa hitaji la msingi la kuhimiza ujenzi wa soko kuu la nchi nzima ni lazima kuwa na utaratibu wa kimsingi wa pamoja wa soko, miundombinu ya soko ya pamoja, vigezo vya pamoja vya utendaji wa kazi wa serikali, usimamizi wa soko na utekelezaji sheria wa pamoja, soko la pamoja la biashara ya raslimali muhimu, na kuendelea kupanua hali ya kufungua mlango ndani na nje ya nchi.
"Ni lazima kudhibiti kwa mujibu wa sheria na kanuni ushindani wa viwanda wa bei chini na usiofuata utaratibu, kufanya usimamizi wa pamoja manunuzi ya serikali na mnada na zabuni, kudhibiti taratibu za kuvutia uwekezaji za serikali za mitaa, na kuhimiza kwa nguvu maendeleo ya pamoja ya biashara kwenye soko la ndani na biashara ya soko la nje ya nchi" mkutano huo umesisitiza.
Mkutano huo umesema, ili kuhimiza maendeleo bora ya hali ya juu ya uchumi wa baharini, ni lazima kuweka mkazo zaidi katika ukuaji unaotokana na uvumbuzi, uratibu na ushirikiano wenye ufanisi wa juu, uhuishaji viwanda, mapatano kati ya binadamu na bahari, na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.
Pia umesisitiza kuongeza uungaji mkono wa kisera na kuhimiza mitaji binafsi kushiriki katika uchumi wa baharini.
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma