

Lugha Nyingine
Burundi yaongeza mara nne mavuno ya mpunga kwa uungaji mkono wa China
Katibu wa Waziri wa Mazingira, Kilimo na Ufugaji nchini Burundi, Leonard Butoyi amesema, nchi hiyo imeongeza mara nne uzalishaji wa mpunga kutokana na uungaji mkono wa kiufundi wa China ambao umekuwa ukitolewa nchini humo tangu mwaka 2009.
Butoyi amesema hayo jumatatu wiki hii wakati wa hafla ya kutoa vyeti kwa Warundi waliopewa mafunzo katika mbinu za kilimo cha kisasa iliyofanyika kwenye kituo cha utafiti wa mpunga cha Gihanga kilichopo Jimbo la Bubanza, magharibi mwa Burundi.
Amesema kutokana na uungaji mkono wa kiufundi wa China, uzalishaji wa mpunga umeongezeka kutoka tani 3 hadi karibu tani 12 kwa hekta moja katika majimbo ambayo kilimo hicho hufanyika kwa uungaji mkono huo wa kiufundi wa China.
Naye Balozi wa China nchini Burundi Zhao Jiangping amerejea tena ahadi ya China ya kuunga mkono maendeleo ya sekta ya kilimo nchini Burundi, akisema kuwa China iko tayari kubadilishana uzoefu wake katika sekta hiyo na watu wa Burundi.
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma