Afrika CDC yapongeza ushirikiano wa afya na China

(CRI Online) Juni 26, 2025

Mkurugenzi wa Kikanda wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) Lul Riek ameipongeza China kwa kuwa mshirika muhimu wa afya wa Afrika.

Akizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua jana Jumatano pembezoni mwa mkutano wa nne wa mwaka wa taasisi za kitaifa za afya ya umma (NPHI) kwa ajili ya kanda ya Kusini mwa Afrika uliofanyika katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, Riek amesema China imetoa uungaji mkono mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya.

“China ni mshirika bora sana kwa kazi ya Afrika CDC. Miundombinu yetu ya kupendeza ya operesheni za dharura na makao makuu ya Afrika CDC nchini Ethiopia imewezekana kwa sababu ya ushirikiano tulionao na China” amesema.

Bw. Riek pia ametoa wito wa ushirikiano zaidi na China katika kuunga mkono nchi za Afrika zenye miundombinu ya afya ya umma, uwezo wa mafunzo kwa wafanyakazi wa maabara na ujenzi wa taasisi za afya ya umma.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha