

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu Li asema China ina imani na uwezo wa kudumisha ukuaji wa kasi wa uchumi
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa 16 wa Mwaka wa Mabingwa Wapya, unaojulikana pia kwa jina la Jukwaa la Uchumi Duniani la Majira ya Joto la Davos, mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Juni 25, 2025. (Xinhua/Rao Aimin)
TIANJIN - China ina imani na uwezo wa kudumisha ukuaji wa kasi wa uchumi, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema jana Jumatano wakati akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa 16 wa Mwaka wa Mabingwa Wapya, unaojulikana pia kwa jina la Jukwaa la Uchumi Duniani la Majira ya Joto la Davos, katika Mji wa Tianjin, kaskazini mwa China.
"Katika miaka mingi iliyopita, haijalishi namna gani mazingira ya kimataifa yalivyobadilika, uchumi wa China umeendelea kudumisha mwelekeo wake mzuri" Li amesema.
Amesema kuwa Pato la Taifa la China (GDP) liliongezeka kwa asilimia 5.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2025 katika hali ya kukabiliwa na mshtuko mkubwa wa nje mwaka huu.
"Viwango muhimu vya uchumi vimeendelea kuimarika katika robo ya pili, na nimeona kwamba taasisi za kimataifa hivi karibuni zimeongeza matarajio yao kwa ukuaji wa uchumi wa China," amesema, akiongeza kuwa maendeleo ya uchumi wa China si kuhusu kasi ya muda mfupi, bali ni maendeleo ya hatua kwa hatua kwa kuelekea malengo ya muda mrefu.
Pia ameeleza kuwa China inasonga mbele kuelekea kuwa nchi yenye mapato ya juu kwa watu wa ujumla, ikichochewa na mahitaji makubwa ya kupanda ngazi kwa matumizi katika soko la pili kwa ukubwa duniani la wanunuzi na uagizaji bidhaa.
Waziri mkuu huyo amesema, "China inajitahidi kujiendeleza yenyewe kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya matumizi kwenye msingi imara wa nchi yenye nguvu ya viwanda vya utengenezaji wa bidhaa," na mafanikio na maendeleo ya hatua kwa hatua ya China katika uvumbuzi yataingiza uhai mpya kwenye maendeleo ya dunia nzima na kusaidia kukabiliana na ukuaji wa kudidimia wa uchumi duniani kote.
Kwenye mkutano huo wa Davos uliopangwa kufungwa leo Alhamisi, Rais wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) Borge Brende ametoa matarajio ya matumaini juu ya uchumi wa China.
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair pia amesisitiza simulizi ya aina yake ya China kuhusu mabadiliko ya muundo wa uchumi katika miongo ya hivi karibuni, akitoa wito kwa nchi mbalimbali kuielewa China na kuendelea kushirikiana na China, badala ya kuitenga.
Ukifanyika chini ya kaulimbiu ya "Ujasiriamali kwa Zama Mpya," mkutano huo ulioanza juzi Jumanne Juni 24 na kumalizika leo Juni 26, umevutia watu maarufu zaidi ya 1,700 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 90 kujadili namna ujasiriamali na teknolojia zinazoibuka zinavyoweza kufungua uhai wa uchumi wenye ustawi na himilivu zaidi.
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma