

Lugha Nyingine
China kuongeza uungaji mkono kwa mambo ya fedha, ili kuhimiza matumizi
Watu wakitembelea Eneo la Chapa za Ndani la Maonyesho ya 5 ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China (CICPE) mjini Haikou, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Yang Guanyu)
BEIJING - China imetangaza miongozo juu ya kuhamasisha uungaji mkono kwa mambo ya fedha ili kuongeza ipasavyo matumizi, ambapo miongozo hiyo, kwa pamoja iliyotolewa na vyombo sita vya serikali ikiwemo Benki Kuu ya China, inaelezea hatua mbalimbali zinazolenga maeneo muhimu ya matumizi.
Waraka huo unatoa wito wa uungaji mkono mkubwa wa mambo ya fedha kwa vyote matumizi ya bidhaa na huduma.
Miongozo hiyo inapendekeza hatua 19 muhimu kutoka vipengele sita, ikiwemo kuunga mkono kuimarisha uwezo wa matumizi, kupanua usambazaji fedha katika sekta ya matumizi na kutumia kikamilifu nguvu bora za matumizi ya wakazi.
Miongozo hiyo inaeleza kuwa ni muhimu kuimarisha msingi wa uchumi mkuu na mambo ya fedha ili kusaidia ukuaji wa mapato ya ajira kwa wakaazi na kuongeza mahitaji ya matumizi.
Inafafanua kuwa, mamlaka husika zitaimarisha motisha ya zana za sera za kimuundo za mambo ya fedha, kuongeza uungaji mkono wa mikopo kwa maeneo muhimu ya matumizi ya huduma, na kuendeleza njia mbalimbali za kifedha kama vile bondi na umiliki hisa na mali.
Waraka huo unasema kuwa, mengi zaidi yatafanywa ili kuongeza uungaji mkono wa kifedha katika maeneo muhimu ya matumizi, kuvumbua bidhaa za mambo ya fedha kulingana na mazingira ya matumizi, na kuhimiza ufanisi wa huduma za mambo ya fedha katika sekta ya matumizi.
Miongozo hiyo inasisitiza kuwa, China itaboresha zaidi huduma za malipo ya watumiaji, kuboresha ujenzi wa mfumo wa mikopo katika sekta ya watumiaji, na kuimarisha ulinzi wa haki za kifedha za watumiaji.
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma