

Lugha Nyingine
Syria yasema IS inabaki kuwa tishio kubwa zaidi kiusalama baada ya shambulizi la kujitoa mhanga kanisani
Msemaji wa mamlaka za mambo ya ndani za Syria Noureddin al-Baba (Nyuma) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Damascus, Syria, tarehe 24 Juni 2025. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)
DAMASCUS - Kundi la IS na masalia ya makundi mengine yenye msimamo mkali yanabaki kuwa changamoto kubwa zaidi kiusalama kwa Syria, msemaji wa mamlaka za mambo ya ndani za Syria Noureddin al-Baba amesema jana Jumanne, kufuatia kukamatwa kwa washukiwa wanaohusishwa na shambulizi la kujitoa mhanga katika Kanisa la Mar Elias mjini Damascus.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Damascus, al-Baba amesisitiza kuwa IS inaleta tishio la kuvuka mpaka ambalo linahatarisha nchi kadhaa, siyo Syria pekee.
Mamlaka za mambo ya ndani za Syria zilitangaza mapema Jumatatu kwamba zilikuwa zimebomoa kundi lenye mafungamano na IS lililohusika na shambulizi hilo la bomu la kujitoa mhanga siku ya Jumapili kwenye kanisa hilo katika kitongoji cha Dweilaa, ambalo limeua watu takriban 25 na kujeruhi zaidi ya 60. Shambulizi hilo ni la baya zaidi kuwahi kutokea katika mji mkuu wa Syria katika miaka mingi iliyopita.
Kwa mujibu wa al-Baba, hatua mbalimbali zimetekelezwa katika maeneo ya vijijini Damascus kufuatia shambulizi hilo la bomu la kujitoa mhanga, na kukamata kundi zima, vilevile vifaa vya vilipuzi na silaha na amethibitisha kwamba kundi hilo lilikuwa likifanya kazi kwa kujitegemea bila kutumika na mamlaka yoyote ya kidini ya eneo hilo.
Al-Baba amesema kuwa mahojiano na mwanamgambo aliyetekwa yameongoza mamlaka husika hadi kwenye maeneo ya maficho yote ya kundi hilo na amemtaja kiongozi wa kundi hilo kuwa ni Mohammad Abdel-Ilah al-Jumaili, anayejulikana pia kwa jina la Abu Imad al-Jumaili, raia wa Syria kutoka eneo la al-Hajar al-Aswad la Damascus na mtu maarufu wa zamani wa IS anayejulikana kwa jina la "gavana wa jangwa"
Washambuliaji wawili wanaotajwa kuwa nyuma ya shambulizi hilo la Kanisa, akiwemo mmoja aliyerusha fulana yake ya vilipuzi ndani ya Kanisa la Mar Elias na mwingine aliyekamatwa akiwa njiani kuelekea kwenye kaburi la Sayyida Zainab Shiite pembezoni mwa Damascus, walikuwa ni raia wa kigeni walioingia Syria kupitia jangwani baada ya kutoroka kutoka kambi ya al-Hol.
Msemaji huyo amesema IS iliwaajiri kama sehemu ya juhudi za kutumia kikamilifu pengo la kiusalama kufuatia mpito wa hivi karibuni katika utawala wa Syria.
Skrini ikimwonyesha anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la IS, anayetambuliwa kwa jina la Mohammad Abdel-Ilah al-Jumaili, kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Damascus, Syria, tarehe 24 Juni 2025. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)
Msemaji wa mamlaka za mambo ya ndani za Syria Noureddin al-Baba (wa kwanza kulia) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Damascus, Syria, tarehe 24 Juni 2025. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)
Msemaji wa mamlaka za mambo ya ndani za Syria Noureddin al-Baba akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Damascus, Syria, tarehe 24 Juni 2025. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma