Kampuni tatu za China zasaini makubaliano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kuendeleza mafunzo na uvumbuzi

(CRI Online) Juni 24, 2025

Kampuni tatu za China zimesaini makubaliano ya maelewano na Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania ili kuongeza ushirikiano kwenye sekta za mafunzo, ushiriki wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi na wafanyakazi, na ushauri wa kiteknolojia.

Mkurugenzi wa China wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Zhang Xiaozhen amesema, makubaliano hayo yaliyosainiwa na kampuni tatu za CRJE tawi la Afrika Mashariki, LETS KZJ na JUYE Saruji, yanalenga kuunga mkono mradi wa mafunzo ya wahitimu kwa wanafunzi wa chuo kikuu, na kutoa fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza na ya uzamili.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu Mkuu wa UDSM Profesa William Anangisye amesisitiza kuwa makubaliano hayo yatawapatia wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho fursa kubwa ya kuongeza uelewa mkubwa kuhusu sekta halisi ya uhandisi na ujenzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha