

Lugha Nyingine
Muundo wa medali za Michezo ya Dunia ya Chengdu 2025 waoneshwa kwa umma
Muundo wa medali za Michezo ya Dunia ya Chengdu 2025 ukiwa umeoneshwa kwa umma tarehe 19 Juni, 2025. (Picha kwa hisani ya IWGA)
CHENGDU, China - Muundo wa medali za Michezo ya 12 ya Dunia, ambayo itafanyika Chengdu mwezi Agosti mwaka huu, umeoneshwa kwa umma mjini Chengu, mkoani Sichuan jana Alhamisi ambapo medali hiyo imepewa jina la "Zhuguang," ambayo tafsiri yake halisi ni "mwanga wa mwanzi," na pia ikitamkika kama "kukimbiza mwanga" kwa lugha ya Kichina.
Ukiwa imechochewa na utamaduni wa wenyeji na kukita mizizi katika falsafa ya kunufaishana, muundo huo wa medali una vitu vikiwemo motifu ya Ndege wa Jua wa Dhahabu (Golden Sun Bird) na panda, alama zinazohusiana kwa ukaribu na Chengdu.
Medali hiyo pia inaweka pini inayoweza kutolewa katikati yake, ambayo wanamichezo wanaweza kuitoa zawadi kwa mtu muhimu, anayebeba moyo wa shukrani na muungano.
Sehemu ya mbele ya medali hiyo ina nembo ya Shirikisho la Kimataifa la Michezo ya Dunia, ikiwa imezungukwa na jina la michezo hiyo kwa Kichina na Kiingereza.
Ukiwa umechorwa kwa mistari ya kontua inayotiririka ya mandhari ya mji huo wa Chengdu na muundo wa kale wa Ndege wa Jua wa Dhahabu, muundo huo unaleta mazingira yenye mwanga, ukiashiria ustaarabu wa Wachina na mwako wa kudumu wa moyo wa michezo.
Miundo ya mbele na nyuma ya medali ya Michezo ya Dunia ya Chengdu 2025. (Picha kwa hisani ya IWGA)
Upande wa nyuma, nembo rasmi ya Michezo hiyo imewekwa juu ya mianzi, ambayo inaonyesha uhimilivu na uadilifu katika utamaduni wa China.
Mchoro wa mianzi, pamoja na picha ya "Shubao", panda maskoti, unalenga kueleza maadili ya msingi ya Michezo hiyo ya amani na urafiki kupitia mchezo.
Sehemu ya katikati ya medali kuna hibiscus, ua la mji wa Chengdu, ambalo ni alama ya urafiki wa kudumu na uhai wenye hamasa wa michezo ya China.
Utepe wa medali una picha za Ndege wa Jua wa Dhahabu, kinyago cha dhahabu cha kuvaa usoni cha Sanxingdui, na ua la hibiscus. Unachukua kazi za kudarizi za Shu, urithi wa utamaduni usioshikika wa China.
Michezo ya Dunia 2025 itafanyika kuanzia Agosti 7 hadi 17.
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma