Rais Xi asema kusimamisha vita ni hitaji la dharura sasa kwa Mashariki ya Kati Wakati wa kuzungumza na Putin

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 20, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Alhamisi katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais wa Russia Vladimir Putin ambayo viongozi hao wawili walibadilishana maoni kuhusu hali ya sasa ya Mashariki ya Kati, amesema kuwa kusimamisha vita lazima ni hitaji la dharura katika Mashariki ya Kati.

Rais Xi ameelezea kanuni na msimamo wa China, akisema kuwa hali ya sasa ya Mashariki ya Kati ni hatari sana, ikionesha zaidi kwamba dunia inaingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko.

"Kama mgogoro utaendelea kupamba moto, si tu pande zinazohusika moja kwa moja zitapata hasara kubwa zaidi, bali pia nchi katika eneo zima zitaathiriwa vibaya," Rais Xi amesema.

Amesema kutumia nguvu ya kisilaha si njia sahihi ya kutatua migogoro ya kimataifa na kutaweza tu kuzidisha chuki na makabiliano.

"Pande husika katika mgogoro huo, hasa Israel, zinapaswa kusitisha operesheni za kijeshi haraka iwezekanavyo ili kuepusha kupamba moto kwa mgogoro na kuzuia kithabiti vita kuenea kwa nje ya eneo hilo," Rais Xi amesema.

Rais Xi pia amesema kuhakikisha usalama wa raia lazima ni muhimu zaidi, na mstari mwekundu wa kulinda raia katika migogoro ya kisilaha lazima usivukwe wakati wowote, na kutumia nguvu ya kisilaha kiholela hakukubaliki.

Ametoa wito kwa pande husika katika mgogoro huo kufuata kwa makini sheria za kimataifa, kuepuka kudhuru raia wasio na hatia, na kuwawezesha raia wa nchi za upande wa tatu wanaondoka kwa usalama.

Rais Xi amehimiza pande husika kuunga mkono kithabiti kutatua suala la nyuklia la Iran kwa njia ya kisiasa, na kuhimiza suala hilo kurudi kwenye njia ya ufumbuzi wa kisiasa ili kutatuliwa kwa kupitia mazungumzo na majadiliano.

Rais Xi amesema kuwa mgogoro huo kati ya Israel na Iran umesababisha hali ya Mashariki ya Kati imezidi kuwa mbaya zaidi kwa ghafla na kuathiri vibaya usalama wa dunia nzima.

"Jumuiya ya kimataifa, hasa nchi kubwa ambazo zina ushawishi maalum kwa pande husika kwenye mgogoro huo, zinapaswa kufanya juhudi za kutuliza hali hiyo, si kinyume chake," amesema, akitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuonesha umuhimu wake zaidi katika suala hilo.

Kwa upande wake Rais Putin ameelezea maoni ya Russia kuhusu hali hiyo ya sasa ya Mashariki ya Kati, akisema kuwa, mashambulizi ya Israel dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran ni hatari sana.

"Kupamba moto kwa mgogoro huo hakulingani na maslahi ya yeyote," amesema rais huyo wa Russia, na suala la nyuklia la Iran linapaswa kutatuliwa kwa kupitia mazungumzo na majadiliano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha